JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
|
UBORESHAJI
WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
MIKOA YA
GEITA,
SIMIYU, MWANZA, SHINYANGA, ARUSHA , KILIMANJARO, MARA NA MANYARA .
Zoezi hilo la Uboreshaji litanzia tarehe
09/06/2015 hadi 09/07/2015.
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vitongoji,
Mitaa na Vijiji katika Kata zote za Mikoa hiyo mine iliyotajwa.
Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na
kufungwa saa 12:00 jioni
Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-
·
Waliotimiza
umri wa Miaka 18 na watakaotimiza Miaka
18 ifikapo mwezi Oktoba 2015.
·
Waliojiandikisha
awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuhuisha taarifa zao na
kupata kadi mpya za kupigia kura.
·
Wote
ambao wanazo sifa lakini hawajawahi kujiandikisha
·
Wananchi
wanatakiwa kwenda kujiandikisha kwenye vituo vya kujiandikisha vilivyoko
ndani ya Kata zao.
Uandikishaji utafanyika kwa muda wa siku saba (7) kwa
kila kituo.
JITOKEZE SASA NENDA
KAJIANDIKISHE
Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, +255 772 55 55 53
S.L.P. 10923, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment