Wafanyakazi wa Airtel Tanzania wakiwahudumia
chakula watoto wenye mahitaji maalum katika hafla ya kukabidhiwa darasa jipya
lililojengwa kwa udhamini wa Wafanyakazi hao kama sehemu ya huduma kwa jamii kwa
ajili ya watoto hao, katika Shule ya Msingi Pongwe jijini Tanga jana.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
• Wasanii king kikii na Banana
zoro washiriki kuchangisha pesa za ujenzi
• Ujenzi na samani vyagharimu milioni 28.
• Ujenzi na samani vyagharimu milioni 28.
WAFANYAKAZI wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja na wasanii wakongwe nchini King kikii na Banana Zolo wameshirikiana kukusanya fedha na kujenga darasa la kisasa litakalotmiwa na watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Pongwe yenye wanafunzi wapatao 1000 nje kidogo ya jiji la Tanga.
Akikabidhi msaada huo katika hafla iliyofanyika
shuleni hapo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Airtel, Bi.
Adriana Lyamba, alisema msaada huo umewezekana kwa kupitia mradi wa kampuni hiyo
wa kuisaidia jamii wa “Airtel Tunakujali” unaoungwa mkono kwa michango ya
wafanyakazi wake kwa kushirikia na marafiki na wadau mbalimbali.
Leo wafanyakazi wa Airtel kitengo cha huduma kwa
wateja tumefanikiwa kubadili mtazamo wa shule hii ya Pongwe kwa kuwajengea
jengo la kisasa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wapatao 45 na madawati mapya
32.
Alisema kampuni ya Airtel imekuwa ikitilia mkazo
maendeleo ya vijana hapa nchini. Hivyo shule ya Pongwe imekuwa miongoni mwa
shule zilizoweza kuingia katika mfuko wa mradi wa “Airtel Tunakujali” ili kuinua
kiwango cha elimu hapa nchini.
“Lengo la mpango huu ni kuboresha mazingira ya
wanafunzi na walimu mashuleni. Tukiamini kuwa elimu bora huchochewa na
mazingira bora ya kujifunzia wak wanafundzi nay a kufundishia kwa walimu,”
alisisitiza Lyimba.
Kwa upande wake Mwalimu wa watoto wenye mahitaji
maalum wa shule hiyo bw, Yahaya Mwachalika amesema, “jengo hilo ni Faraja
kubwa kwetu na wanafunzi wa Pongwe kwani kwa muda mrefu tumekuwa
tukisomea nje kutokana na uhaba wa madarasa. Msaada huu ni mkombozi kwetu kwani
kwa sasa wanafunzi wetu wa awali watakuwa na mahala pazuri kwa kusomea na kuondokana
na adha ya kujifunza wakiwa nje.
“Kwa niaba ya walimu, wazazi na wanafunzi wa shule
ya msingi ya Pongwe napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kuweza kututengenezea
darasa lililobora na imara. Kutokana na msaada huu tuanaamini kabisa idadi ya watoto
itaongezeka kwa sasa na wazazi watapata moyo zaidi wa kuwaandikisha watoto wao
hapa shuleni hasa ukizingatia wengi wa wanafunzi wetu wanchangamoto
zinazotokana na ulemavu. ”, alisema bw. Mwachalika.
No comments:
Post a Comment