Afisa
Uhusiano Airtel, Jane Matinde akimkabithi vifaa vya michezo Mwenyekiti kamati
ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Nyenza
kwaajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising
Stars, inayotegemea kutimu vumbi kuanzia Ijumaa, Julai 24, 2015 mkoani Mbeya.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi jezi kwa timu za wasichana na
wavulana za U-17 zinazoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars ambayo
inatarajiwa kuanza katika ngazi ya mkoa Ijumaa, Julai 24.
Mkoa
wa Dar es Salam unajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke huku
timu nyingine zikitoka mikoa ya Morogoro, Mbeya, Arusha na Mwanza. Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo
ya soka la Vijana ya TFF Ayoub Nyenzi alisema kwamba maandalizi yote kwa ajili
ya michuano hiyo ngazi za mikoa yamekamilika.
“Ni
matarajio yetu kuwa tutashuhudia mechi zilizojaa ushindani na mvuto na vilevile
ningependa kuona mamlaka zinazohusika na usimamizi wa michuano hiyo ngazi ya
mkoa zikichagua wachezaji bora ambao wataunda timu za kombaini za mikoa tayari
kwa kushiriki fainali hizo ngazi ya taifa zitazofanyika jijini Dar es Salaam
baadaye mwezi Septemba”,alisema.
Mkoa
wa Mbeya utakuwa wa kwanza kuzindua mashindano yake Julai 24, ikifuatiwa na
mkoa wa Dar es Salaam Julai 27, Morogoro Agusti 1 na Arusha Agusti 9, huku
Mwanza wakitarajia kufanya uzinduzi wao mnamo Agusti 15. Wageni rasmi katika
hafla za uzinduzi wa mikoa wanatarajiwa kuwa wakuu wa mikoa husika.
Mikoa
yote shiriki inatarajiwa kuwa na timu za wavulana na wasichana isipokuwa mkoa
wa Arusha ambao unatoa timu ya wasichana pekee na Morogoro inayoshirikisha
wavulana tu. Huu ni mwaka wa tano mfululizo ambao michuano hii imekuwa
ikifanyika nchini, huku ikichangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa vipaji
vyenye manufaa kwa Taifa.
Ofisa
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde, ameelezea nia ya dhati ya kampuni
yake kuendelea kudhamini programu za vijana huku akiomba sapoti kutoka kwa TFF,
Wizara inayoshughulikia masuala ya michezo pamoja na wadau wengine wa mchezo wa
soka.
Alisema
Airtel Rising Stars mwaka huu inaenda bega kwa bega na kampeni mpya ya ‘It’s
Now’ huku nahodha wa Ivory Coast ambaye pia ni kiungo wa Manchester City Yaya
Toure akiongoza kampeni hiyo. Kampeni hii inalenga kulea na kukuza vipaji
barani Afrika kupitia nyanja mbalimbali kama vile michezo, mtindo wa maisha na
mziki lakini vilevile kuwapa mbinu zitazaowawezesha kupata ufumbuzi wa masuala
ya kiteknolojia na kuona fursa zinazowazunguka.
Airtel
Rising Stars ni program ambayo ipo bara zima la Afrika maalum kwa ajili kuwapa
vijana fursa ya kuonesha vipaji vyao na kuwarahisishia makocha kupata vijana
ambao watawaendeleza vipaji vyao kwa manufaa ya baadaye.
No comments:
Post a Comment