Tangazo

Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

May 17, 2018

WAZIRI DK. MWAKYEMBE AZINDUA COPA UMISSETA MJINI BUKOBA

 Waziri Mwakyembe akigawa vifaa vilivyotolewa na Coca-Cola kwa moja ya mwakilishi wa mmoja wa shule za sekondari.
 Waziri Mwakyembe akikagua moja ya timu wakati wa hafla ya uzinduzi.
 Wadau wa Umisseta katika picha ya pamoja na Waziri Mwakyembe.
 Waziri Mwakyembe akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo. Pembeni ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Said Kiganja.
 Waziri Mwakyembe akiongea na wanafunzi waliohudhuria.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mhandisi Richard Ruyango akiongea wakati wa hafla hiyo.
Waziri Mwakyembe akijiandaa kupiga penati  wakati wa uzinduzi huo. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta mjini Bukoba. Akizindua mshindano hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Dkt. Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema michezo ni burudani, inaleta undugu, umoja na upendo hivyo h aina budi kuienzi siku zote.

 "Nawaomba vijana mpende michezo maana ni burudani na ilateta afya kwa watu wa rika zote, mkizingatia hivyo hakutakuwa na watu wenye magonjwa ya ajabu ajabu," amesema. Mashindano hayo yalipambwa na shamrashamra mbalimbali za michezo na burudani katika uwanja wa Kaitaba na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa michezo na wanzi wa shule za sekondari na mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyango, aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Said Kiganja.

May 11, 2018

COASTAL UNION YAMKABIDHI TUZO YA HESHIMA WAZIRI UMMY MWALIMU

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akipokea tuzo ya heshima  ya kutambua mchango wake kwa kuipandisha timu ya Coastal Union kucheza Ligi kuu msimu ujao kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu hiyo Salimu Bawaziri mapema leo kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati alipofungua mashindano ya Ligi ya Banda Cup .   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akionyesha waandishi wa habari tuzo aliyokabidhiwa na klabu ya Coastal Union kwa kutoa mchango wake kuipandisha kucheza Ligi kuu msimu ujao kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga (CCM) Azzah Hamadi Hilali Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)kushoto akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri ikiwa ni kutambua mchango wake wa kuisaidia timu hiyo kuweza kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao tuzo hiyo walikabidhiwa pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano January Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli(CCM) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM),Asas ya Iringa na Mo Dewji. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

May 9, 2018

UZINDUZI WA COPA UMISSETA SINGIDA WAFANA

 Wawakilishi wa shule za sekondari wakipokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Coca-Cola kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahia zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akijiandaa kupiga penati wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo.

May 7, 2018

MBIO ZA MBEYA TULIA MARATHON ZAFANA JIJINI MBEYA

Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizindua mbio za Kilometa 45, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni.  Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akiongoza mbio za Kilometa Tano, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Wadau wakishiriki mbio hizo
Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 100 kwa upande wa wanawake, Nasra Abdallah, akimalizia mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Mshindi wa Marathoni ni Abraham Too alikimbia 2:42:02:08, Francis Bowen wote wa Kenya 2:42:02:73 na Nestory Steven aliyekimbia saa 2:45:39, Ambapo wa kwanza alipata Sh milioni 3, wa pili milioni 2 na watatu milioni 1.
Wanawake  ni:- 
Nusu marathoni ni Failuna Abdi, Christina Kambua wa Kenya na Adelina Trazias wa Tanzania, kwa wanaume ni Bernard Musau wa Kenya, Paschal Mombo wa Tanzania na George Olihaki wa Kenya. Ambapo mshindi alipata sh milioni 2  wa pili wa pili 700,000 na watatu 500,000.
Kwa upande wa mbio za Baiskeli bingwa ni Richard Laizer, Hamis Hussein na Masunga Duba, kwa wanawake ni Sophia Khatimu, Lawlence Luzuba na Habibu Mathias
Mita 1500 ambao walivikwa medali na Nanai ni James  John, Geofrey Edison, Yeli Adam kwa wanawake ni Sarah Ariko, Omega Elia na Silvana Elias
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizindua mbio za Kilometa 45, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizindua mbio za Kilometa 21, wakati wa Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akiwaongoza washiriki mbio za Kilometa Tano, kufanya mazoezi ya kujiandaa kushiriki Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Wadau wakipozi kwa picha
Mshindi wa tatu Kilometa 45 kwa wanawake kutoka Kenya akimalizia mbio
Wazee wakijifua kabla ya kuanza kutimua mbio za Kilometa mbili
Washiriki wa mbio za wazee za Kilometa mbili wakianza kutimua mbio
Baadhi ya washiriki wakifanya mazoezi ya kujiandaa na mbio
Mpigapicha wa Azam Tv, akiwa kazini kupata matukio ya mbio hizo kwa kutumia usafiri wa Bodaboda
Mwakilishi wa Kampuni ya Derm Electrics, Irene na Mtangazaji wa Redio ya Mbeya Fm, Gwamaka Mwankota, wakishiriki mbio hizo.
Wawakilishi kutoka DSTV wakishiriki mbio za Kilometa tano
Mhes Dkt. Tulia akiwaongoza washiriki wa mbio za Kilometa tano kumaliza mbio hizo.
Kutoka (kushoto) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Farid Kubanda Fid Q, Sebastian na Barbara kutoka Clouds pamoja na mwakilishi wa Tatu Mzuka, wakiwa katika Uwanja wa Sokoine kushuhudia mbio hizo.
Mshindi wa pili wa mbio za Kilometa 45 kwa upande wa wanawake, Sarah Ramadhan, akimalizia mbio hizo 
Mshindi wa pili wa mbio za Kilometa 45 kwa upande wa wanawake, Sarah Ramadhan, akibebwa na wasaidizi baada ya kuzidiwa na kuishiwa nguvu wakati akimalizia mbio hizo za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni.
Mshindi wa pili Kilometa 21 akimalizia mbio
Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 100 kwa upande wa wanaume, akimalizia mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo na kushirikisha wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti na Makampuni. 
Wakimbiaji wa Kilometa 500 wakianza kutimua mbio
Marry Naali akimalizia mbio za Kilometa 800 na kushika nafasi ya kwanza
 Wadau katika pozi la picha
 Washiriki kutoka CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na Naibu Spika
 Mafoto naye hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo za kilometa tano
  Naibu Spika, Dkt. Tulia akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amosi Makala.