Timu ya Mariado wakishangalia ubingwa kwa staili ya aina yake
baada ya kuibuka mabingwa wa michuano ya Airtel Rising Star, jana jijini
Arusha.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Timu ya wasichana ya Mariado yanyakua ubingwa katika mashindano ya vijana chini
ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stas mkoa wa Arusha baada ya kuibamiza
Crisking mabao 3 – 0, katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi
ya Meru.
Timu zote zilianza kwa kasi lakini kadri muda ulivyozidi kwenda Crisking
walipoteza umakini na kuwapa nafasi wapinzani wao kushinda mchezo huo. Mariado
walipata magoli kupitia kwa Mariam Rashid aliefunga magoli mawili na Caroline
Antipace alietimisha kwa kufunga goli la siku.
Akiongea katika sherehe za kufunga katibu wa chama cha mpira wa miguu Adam
Brown aliipongeza timu ya wasichana ya Mariado kwa kuchukua ubingwa na kuwataka
kufanya juhudi zaidi. “ huu ni mwanzo tu katika kazi yenu na mnapaswa kuongeza
juhudi ili ndoto zenu zitimie za kua wachezaji nyota”, alisema Brown.
Amepongeza wadhamini wa mashindano kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuendelea
kutoa mchango katika mpira wa miguu Tanzania. “Mpira unaihitaji fedha ili uweze
kuendelea. Tunashukuru sana kwa msaada wa fedha ambao tunaupata kutoka Airtel
Tanzania katika kuendesha programu hii kwa vijana,” alisema.
Kumalizika kwa michuano hii ngazi ya mkoa inatuleta karibu na fainali za taifa
zitakazo fanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar-es-Salaam
kuanzia September 11 mpaka 21. Timu ya kombaini ya Arusha itashiriki michuanao
ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa pamoja na timu za Ilala, Temeke,
Kinondoni, Mbeya na Mwanza.
Timu za wavulana zinashirikisha Ilala, Temeke, Kinondoni, Morogoro, Mbeya na
Mwanza. “Naamini vipaji vinavyozalishwa na Airtel Rising Stars kila mwaka vitalipeleka taifa hili katika Mafanikio makubwa,” Alisema Brown.
Akizungumza katika hafla hiyo muwakilishi wa Airtel, Nassoro
Laizer aliwashukuru viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa Arusha kwa muda wao
na kushiriki kikamilifu katika mashindano na kusisitiza kuendelea kudhamini
program hii ya kusaka vipaji.
Aliwataka wachzaji wa timu za wasichana kutumia vizuri fursa hii
ya Airtel Rising Stars ili waweze kutimiza ndoto zao katika soka.
No comments:
Post a Comment