Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea umuhimu waUtafiti wa Afya ya Uzazi na
Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo
ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
XXXXXXXXXXXXXXXX
NA: VERONICA KAZIMOTO,
MOSHI
Wito umetolewa kwa viongozi wote wa
Serikali katika Ngazi zote na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa
Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na
Malaria utakaoanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015.
Wito huo uletolewa leo na
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Ahmed
Makuwani wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika
wilayani Moshi, Kilimanjaro.
"Ninawaomba Wananchi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi, Wasimamizi na Wahaririwatakaoshiriki zoezi
la kukusanya Takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa
mwaka 2015 ili kupata taarifa muhimu na sahihi kwa ajili ya kupanga
Mipango na Sera endelevu za Sekta ya Afya katika nchi yetu, amesema
Makuwani".
Dkt. Makuwani amesema kuwa taarifa
zitakazokusanywa kwa wananchi kwa ajili ya utafiti huo zitakuwa ni
siri na zitatumika kwa shughuli za Kitakwimu tu na wala hazina uhusiano wowote
na Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
kwa upande
wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema
utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 unalenga
kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika kutathmini
malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati mipya.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara
nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa
mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu
utaanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015 kwa nchi nzima na utamalizika mwishoni mwa
Mwezi Februari 2016.
No comments:
Post a Comment