Waziri wa Habari, Utamanduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye
akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016
jijini Dar es Salaam.
|
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano
akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
|
Rais wa TFF Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
|
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa
Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa wa Msimu
wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye leo amezindua msimu wa sita wa mashindano ya
soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars na kuwapongeza
Airtel Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali
pamoja na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) za kukuza mchezo wa soka.
“Programu za soka za vijana ndiyo
muhimili wa maendeleo ya soka popote pale duniani. Ndiyo maana nasisitiza
umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo matunda yake yameonekana
dhahiri katika kipindi cha miaka mitano iliyopita”, alisema
Nnauye.
Alitoa mfano wa timu ya taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambayo wachezaji wake 10 wa
kutumainiwa wametokana na Airtel Rising Stars. “Matunda ya Airtel Rising Stars
vilevile yanaoneka dhahiri kwenye timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo
wachezaji wake wote wanatokana na programu hii ya vijana”, alisema Nnauye.
Klabu za daraja la kwanza na ligi kuu Tanzania bara pia zinafaidi matunda ya
Airtel Risings Stars.
Waziri amewataka viongozi wa soka
kusimamia vizuri pragarmu ya Airtel Rising Stars ili kuweza kubaini vipaji
vingi zaidi kupitia mashindano haya ya vijana ya kila mwaka yakishirikisha timu
za wasichana na wavulana kuanzia ngazi ya mkoa na kuhitimishwa kwa fainali ya
Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alimhakikishia waziri kuwa
kampuni ya Airtel Tanzania ina nia thabiti ya kuendelea kudhamini michuano hiyo
ambayo imesaidia kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo
huo marufu hapa nchini.
Alisema Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa
kampeni ya Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha
vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel
Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana kutumia
vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano cha kipato cha
kuaminika”, alisema.
“Kwa kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar,
Airtel Tanzania tunawiwa kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia
mchezo wa mpira wa miguu ambao ni marufu kuliko michezo yote hapa Tanzania. Ni
njia ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuedelea kutuunga mkono”,
alisema.
Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema programu ya
Airtel Rising Stars imeleta mapinduzi na kubadilsha kabisa sura ya mchezo wa
soka hapa nchini. “Nawapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono.
Naamini kwamba tutapata mafanikio makubwa zaidi siku za usoni”, alisema.
Airtel Rising Stars mwaka huu itashirkisha timu kutoka mikoa ya
Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala, Morogoro (wavulana) wakati mikoa
itakayoshirikisha timu za wasichana ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha,
Lindi na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment