Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) mkoani Kagera, Abdul Kitula (kulia) akimkabidhi bahasha iliyo na majina ya Halmashauri mbili zilizopitishwa kuanza utekelezaji wa mradi wa PS3, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msole mjini Bukoba leo. Halmashauri Mbili za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo ndizo zimechaguliwa kuanza utekelezaji wa mradi huo.Source:Father Kidevu Blog
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msole akionesha bahasha hiyo iliyo na majina.
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Amantius Casmiri Msoleakizisoma Haklamashauri zilizo chaguliwa ambazo ni Wilaya ya Kyerwa na Biharamuloambazo zimeonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kuimarisha mifumo yake kulinganisha na Halmashauri zingine sita za Karagwe, Muleba, Misenyi, Ngara, Bukoba Mji na Bukoba ambazo zitaingia awamu ya pili.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Col (Mstaafu) Shaban Shaban Ilangu Lissu ambaye Wilaya yake imechaguliwa kuanza awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa PS3.
Ofisa kutoka PS3 Soud Abubakar akiwasilisha sifa na vigezo vilivyo tumika kuzipata Halamashauri mbili za awali zilivyo patikana ili ziweze kuanza utekelezaji wa mradi.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa kutoka Wilaya mbalimbali.
Washiriki wakifuatilia uwasilishajki huo.
Mwakilishi wa Halmashauri ya Mji wa Bukoba, ambaye ni Mchumi Msaidizi, Rahel Mbuta akiwasilisha kazi za makundi ambazo ziliainisha Changamato na maeneo ya uboreshaji. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Meneja wa Mifumo ya Habari na Mawasiliano wa Mradi wa PS3, Giovvan Di Piazza akiwajibika kuhakikisha mawasilisho yote yanaenda vyema.
Washiriki wakifuatilia uwasilishaji kutoka katika makundi.
Mwakilishi
wa Halmashauri ya Wilaya wa Bukoba, ambaye ni Mhandisi wa Maji, Ndolimana Kijigo akiwasilisha kazi za makundi ambazo ziliainisha Changamato na maeneo ya
uboreshaji.
Washiriki wakiwamakini kusikiliza mada
Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Imani Mgonja akiwasilisha tarifa ya kundi la Halamashauri yake.
Maofisa kutoka Wizarani wakifuatilia kwa makini mawasilisho hayo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Henrietta William akiwakilisha Halmashauri yake.
Mmoja wa washiriki akiuliza swali kutokana na mawasilisho ya makundi mbalimbali.
Mratibu
wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali
yaliyoulizwa na washiriki.
Ofisa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Debora Mkemwa akifafanua baadhi ya hoja.
Dk Rest Lasway (kushoto) akizungmza na Nanzia Florence wote kutoka PS3.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sebastian Kitiku akichangia na kujibu hoja zilizotolewa.
Mtaalam wa fedha wa PS3 ambaye pia ni Kiongozi wa Uzinduzi wa mradi Mkoa wa Kagera, Abdul Kitula akizungumza.
Mtaalam wa Masuala ya Utawala Bora katika Mradi wa PS3, Paul Chikira akizungumza kwa niaba ya timu nzima ya PS3 iliyopo mkoani Kagera.
Wenyeviti wa Halamashauri za Wilaya za Biharamulo, Hafsa Galiatano na Mwenzake kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Kashunju Runyogote wakisikiliza utangazaji wa Halmashauri zinazoanza mradi ambapo Halmashauri zao zimechaguliwa kuanza. Source:Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment