Tangazo

July 5, 2016

WANANCHI WAZIDI KUMIMINIKA BANDA LA PSPF, MKURUGENZI MKUU AWASAIDIA WAFAMYAKAZI WAKE KUHUDUMIA WATEJA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akiyekaa, akimuonyesha Mwanachama huyu wa Mfuko huo michango yake papo kwa hapo kwenye banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016. Mamia ya Wananchi wamekuwa wakimiminika kwenye banda hilo, ambapo jambp la kuvutia Mkurugenzi Mkuu huyo aliungana na wafanyakazi wake kutoa huduma kwa wananchi. Maonyesho hayo yanashirikisha jumla ya nchi 30 ambapo banda la PSPF limekuwa na idadi kubwa ya wananchi wanaotembelea kujua huduma zitolewazo kwa wananchi ambao si wanachama lakini pia kuwahudumia wanachama wake. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
 Mama Anna Mkapa, (kulia), Mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la EOTF linalokusanya wajasiriamali kutoka mikoa yote ya bara na vuisiwani. Kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, wajasiriamali hao wanaweza kujiunga na Mfuko huo na hivyo kufaidika na mafao mbalimbali yakiwemo ya kuboresha biashara zao
 Mama Salma Kikwete, (kulia), Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, walipokutana kwenye banda la EOTF kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016.
 Mamia ya wananchi wakiwa kwenye banda la PSPF Julai 4, 2016
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo,  Mwanaidi Msangi baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo,  Baturi J. Msusi, baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016
 Baturi J. Msusi mwanachama mpya wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga leo Julai 4, 2016 na kupatiwa papo hapo.
 Mwanaidi Msangi, mwanachama mpya wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga leo Julai 4, 2016 na kupatiwa papo hapo.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, (katikati), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wizarani hapo, Ben Mwaipaja, wakipatiwa maelezo na Afisa wa UTT-AMIS, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwenye jengo la Wizara ya Fedha, viwanja vya Maonyesho ya Biashaya ya Kimataifa Mwalimu Nyerere, Maarufu kama Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimpatia maelezo ya kiutendaji Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, (watatu kushoto), Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele (wapili kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, (kulia), wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango ambayo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iko chini ya wizara hiyo.
 Afisa wa PSPF, Pensila (kushoto), akitoa elimu kwa wanachi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akimuhudumia Mwanachama huyu aliyefika kujua hali ya michango yake kwenye banda la Mfuko huo Julai 4, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (aliyekaa0, akisaidiana na wafanyakazi wake kuhudumia wananchi Julai 4, 2016

No comments: