· Airtel FURSA yawezesha wajasiliamali kuonyesha bidhaa na huduma zao katika bure mwishoni mwa wiki
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA mwisho mwa wiki imewakutanisha baadhi ya wajasiliamali jijini Dar es salaam katika maonyesho maalum ya ‘Airtel FURSA Wajasiliamali Bazaar’ yaliyoandaliwa nje ya kiwanja cha ofisi kuu ya Airtel vilivyoko Morocco kwa leongo la kuwakutanisha wajasilimali hao na wateja mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha kutanua masoko yao na kuuza bidhaa zao.
Baadhi ya wajasiriamali walionufaika na mradi wao wa kijamii wa Airtel FURSA nao walipata nafasi za kuhudhuria na kuonyesha bidhaa zao huku wakiipongeza Airtel kwa kuendelea kuwasaidia kuboresha biashara zao.
“Airtel leo wametusaidia sana sisi kukutana na wajasiliamal wenzetu tukabadilishana ujuzi pamoja na kubadilishana mawasiliano ili tuweze kusaidiana kupeana masoko, vilevile hapa katika jengo tumejipatia wateja wengi sana, hatujaamini kabisa kama tungeweza kuuza hivi, mimi nauza keki nimepata wateja hata wa baadae, kunawenzangu wanaouza Kuku, Mayai, Picha za mapambo ya nyumabani, Mito ya mapambo, Ubuyu, Matunda na Sabuni za kufanyia usafi nyumbani nimefurahi kuona kila mtu ameuza na amejitengenezea wateja wa baadae” alieleza mnufaika wa Airtel FURSA Bi Diana Mushi
Tunawashukuru sana Airtel kwa kutupatia jukwaa hili la kuonyesha bidhaa na huduma zetu kwa wadau mbalimbali na kutuongezea wigo wa soko letu. Alisisitiza Bi Diana
Akitembelea maonyesho hayo mkuu wa wilaya ya kinondoni alieleza kufurahishwa kwake na vijana hao huku akiwahimiza vijana wengine kuanziasha biashara ndogo ndogo ili na kuzisimamia vyema ili kutengeneza ajira kwa vijana wengine wengi nchini
“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi sana ikiwa ni pamoja na ardhi yenye rutuba, wanyama na rasilimali nyingine nyingi na bado vijana wengi wanakabiliwa na janga la kukosa ajira ambalo uwiano wa ukosefu wa ajira kwa vijana unakua kwa kasi kila mwaka. Napenda kuwapongeza sana vijana mlioamua kujikita kwenye ujasiriamali bila kujali changamoto zilizoko katika biashara, nawatia moyo vijana wengine kuiga mfano na kujiajiri wenyewe na kukuza maendeleo ya jamii zetu” alisema Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mh Ally Hapi.
Akionge kuhusu mradi wa Airtel FURSA Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya alisisitiza dhamira ya kampuni yake kuendelea kuwawezesha vijana wajasiriamali nchini kwani wanatambua ndio chachu kubwa ya kuinua maendeleo ya jamii
“Airtel FURSA imejipanga kuendelea kuwawezesha vijana ka ili kuweza kuzikamata fursa zitakazowawezesha kufikia ndoto zao kama ilivyofanya leo kupitia maonyesho haya ya ndani ya biashara ya Airtel FURSA wajasiliamali Bazaar” alisema Bi Singano
Bi Singano alimalizia kusema kuwa “Airtel tunaona fahari kwa kufanikiwa kwa mradi huu ambapo mpaka sasa vijana zaidi ya 5000 wamenufaika na elimu ya ujasiriamali na kati yao zaidi ya vijana 100 waliopo katika makundi na binafsi wamewezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi ili kuongeza uzalisjhaji wenye thamani”.
Mradi wa Airtel FURSA ulianzishwa mwaka jana mwezi wa tano kwa lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali kuweza kukuza biashara zao na kuchochea vijana wengi kujikita kwenye ujasirimali kwa lengo la kuinua uchumi wao na jamii inayowazunguka, pia mradi umelenga kutoa katika elimu ya ujasiriamali kwa vijana ili kuwawezesha kujua jinsi ya kuendesha biashara na namna ya kutatua changamoto za kibiashara na kupata faida zaidi.
No comments:
Post a Comment