Tangazo

December 14, 2016

AIRTEL FURSA YAZIDI KUNUFAISHA VIJANA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando  na maafisa biashara wa Airtel Mtwara Jerry Issaya  na Moses Bhalalusesa wakiongea na mmoja wa wanufaika wa mradi wa Airtel Fursa mkoani Mtwara bi. Prisca Chilumba (aliyesimama) walipomtembelea mnufaika huyo katika saluni yake mpya mkoani Mtwara. Airtel ilifanya ziara hiyo ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha msaada huo ili aweze kutimiza ndoto zake. 

Kushoto ni Katibu wa Lindi Sauti ya Jamii kundi la wajasiliamali la bw, Salum Muunguja- na mwenyekiti wake Shaban Zuberi wakionyesha mmoja kati ya mbuzi 10 wa kisasa walionunua baada ya kuweshwa na mradi wa kijamii wa Airtel Fursa mara baada ya kutembelewa na Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando na meneja biashara wa mkoa huo bw, Saleh safy. Airtel ilifanya ziara hiyo ili kujionea maendeleo yao pamoja na kuboresha  kuboresha msaada wao ili vijana waweze kukabiliana na changamoto zilizojitokeza.

XXXXXXXXXXXX 
LINDI

VIJANA wa mikoa ya Lindi na Mtwara  walioendelezwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wa Airtel Fursa wamesema tayari wameanza kupata mafanikio kutokana na Ongezeko la  Faida za kiuchumi ambazo zinatokana na kuwezeshwa na kampuni hiyo.

Hali hiyo imeonekana baada ya Kampuni ya Airtel Kuwatembelea katika maeneo wanayofanyia Biashara mara baada ya kuwawezesha na kusimamiwa na Viongozi wa Airtel wa mkoani kwa lengo la kutazama changamoto pamoja na mafanikio wanayoyapata.

Mkoani  Mtwara mmoja wa mnufanika anaonekana kuboresha eneo lake la biashara baada ya kufungua ofisi nyingine ili  kujipatia faida maradufu huku kikundi cha Sauti ya Jamii  kilichopo Lindi kinachojishughulisha na shughuli za kilimo na ufugaji kilipokea msaada wa mbuzi 40 kuonekana kupata changamoyo na kuanza upya.

“Tunaishukuru sana Airtel  kwa msaada wa mbuzi 40 pamoja na kutujengea banda la kisasa hapo mwanzo,  tumeeendea vyema lakini tukapatwa na changamoto ya baadhi ya mbuzi wetu kupatwa na ugonjwa na kufa, tulijipanga upya kwasasa tuliuza wale wote kama nyama na sasa tumenunua mbuzi wazuri wanaweza kuzaa mapcha kila mzao, sasa tunaamini tutanza kuona faida alisema” Salum Muunguja-Katibu kundi la Sauti ya Jamii

kwa upande wa mjasiliamali wa Airtel Fursa Mtwara Bi. Prisca Chilumba ambae anafanya ujasiliamali wa Saloon saloon ya kike alisema “Mimi kwa kweli naishukuru sana Airtel Fursa kwa kuniwezesha binafsi nimeweza kujipatia kipato cha kunitosha na hadi sasa nimeweza kuboresha ofisi yangu na kuhamia sehemu kubwa zaidi, pia ninamuda hata kujitangaza na kujitolea kwa wengine kwa lengo la kupanua masoko mkoani hapa”.

Naye meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando anasema changamoto katika ujasiliamali ni hali ya kawaida hivyo vijana waliowengi wanapaswa kujifunza zaidi ili kuweza kujikwamua katika dimbwi la umasikini.

Changamoto kwa mjasiliamali ni kitu cha kawaida sana, sisi Airtel tunafanya ziara za kuzunguka na kufahamu maendelea au changamoto za vijana wote waliosaidiwa na Airtel FURSA ili kujua ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia waendelee kufikia ndoto zao, tayari tumeshapita tumeshaandaa mkakati wa kuwasaidia wote hivyo tunachotaka ni jamii pia kuwaunga mkono vijana hawa ili waweze kufikia malengo waliojiwekea na hatimae kusaidia jamii pia”, alieleza Mmbando

No comments: