Tangazo

March 13, 2017

COCA - COLA YAKAMILISHA SHANGWE JIJINI MBEYA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios (kulia), akigongesha soda ya Coca-Cola na viongozi wengine wa kampuni hiyo kuashiria uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji hicho mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha (kutoka kushoto) ni David Karamagi - Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Nalaka Hettiaratchchi – Mkurugenzi wa Mauzo wa Coca-Cola Kwanza na Gary Pay – Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza Mbeya. Sambamba na uzinduzi wa muonekano mpya, Kampuni ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa zake mkoani Mbeya ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia teknolojia ya kisasa katika kiwanda chake kilichopo Mbeya. Picha zote na Mr. Pengo - MMG-MBEYA.
Wageni waalikwa waliofika kusherekea muonekano mpya wa kinywaji cha Coca-Cola.
---
*Yafunga mitambo ya uzalishaji ya kisasa, boresha huduma za usambazaji wa bidhaa zake
Kampuni ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa zake mkoani Mbeya ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia teknolojia ya kisasa katika kiwanda chake kilichopo Mbeya , sambamba na kununua malori mapya kwa ajili ya kurahisisha usambazaji lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha bidhaa zake zinapatikana katika kila kona ya mkoa huo na maeneo mengine yote ya Nyanda za Juu Kusini.

Kutokana na mkakati wake huu wenye mwelekeo wa kupanua soko lake, kampuni jumamosi hii imefanya tafrija maalum ya kusherehekea mafanikio haya iliyofanyika katika hoteli ya Tughimbe na kuwajumuisha wadau zaidi ya 300 kutoka sekta mbalimbali mkoani humo, wakiwemo wafanyabiashara, mawakala wa usambazaji vinywaji na wanamichezo kutoka klabu ya Mbeya FC ambayo inadhaminiwa na Coca-Cola.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios, alisema upanuzi na kufunga mitambo ya kisasa zaidi katika kiwanda cha Coca-Cola mkoani Mbeya umefanyika wakati muafaka ambapo umeenda sambamba na mkakati wa kujiiimarisha zaidi katika soko la Mkoa huo na maeneo yote ya Nyanda za Juu Kusini na kuhakikisha bidhaa zake zinapatikana kila mahali na wakati wowote lengo likiwa na kuwawezesha wakazi wa Mbeya kufurahia ladha murua ya kinywaji cha Coca-Cola na bidhaa nyingine zinazozalishwa na kampuni.

“Kampuni ya Coca- Cola inayo historia ya kuwepo mkoani hapa kwa muda mrefu, na tumeona ni vyema tukawashirikisha katika mkakati wetu wa mafanikio wenye lengo la kuongeza tija na ufanisi, ambapo tumeboresha kiwanda chetu na pia tumejipanga kusambaza bidhaa zetu kuhakikisha zinawafikia wananchi kwa urahisi na mkakati huu tutautekeleza katika mikoa yote vilipo viwanda vyetu”. Alisema Bwana Gadzios.

Kwa upande wake, Mkuu wa kiwanda hicho cha Mbeya, Gary Pay, alieleza kuwa kiwanda hicho kimefanyiwa ukarabati mkubwa na kufungwa mitambo inayotumia teknlojia ya kisasa ya uzalishaji vinywaji, kujenga mabohari ya kisasa na kununua malori makubwa ya kurahisisha usambazaji bidhaa zake kwa wateja.

Bwana Pay alisema uwepo wa kiwanda hicho umetoa ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa kampuni imekuwa mstari wa mbele kutekeleza miradi ya kusaidia jamii, baadhi yake ikiwa ni kutoa msaada wa madawati kwa shule za serikali na udhamini wa timu ya mchezo wa soka ya Mbeya FC.

Alimalizia kwa kusema kuwa kampuni itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii ambapo katika kipindi cha mwaka huu kampuni imedhamiria kutoa msaada wa madawati 1,000 katika shule za serikali za mkoa humo.

No comments: