Meneja
Mauzo Kanda ya Dar es Salaam Airtel Tanzania Brighton Majwala (kulia)
akimkabidhi vifaa vya mchezo Katibu Mkuu wa Chama cha Soka wilaya ya Kinondoni
(KIFA) Funia A. Funia (kushoto) kwa ajili ya mashindano ya Chipukizi Cup
yanayotarajiwa kuanza Octoba 8 kwenye viwanja vine vya wilaya hiyo. Wa pili
kushoto ni Katibu wa mashindano ya vijana wa wilaya hiyo Abdallah Singano na
Meneja Miradi Airtel Tanzania, Jane Matinde.
………………………………………………………
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa
msaada wa vifaa vitakavyotumika kama zawadi katika mashindano ya vijana chini
ya umri wa miaka 17 yajulikanayo kama Chipukizi Cup yanayotegema
kutimua vumbi tarehe 8 october 2017 katika wilaya ya kinondoni.
Mashindana hayo yanayoshirikisha timu 64 kutoka
katika wilaya ya Kinondoni yatatoa fursa kwa vijana kuchuana vikali , kujifua
na kujiweka sawa katika kuchezea vilabu mbalimbali na hatimae kukuza
kiwango cha mpira nchini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo
Meneja Masoko kanda ya Dar es saalam , Brighton Majwala alisema “ leo hii
tunaungana na chama cha mpira wa soka wilaya ya Kinondoni katika kudhamini
mashindano haya kwa lengo la kuwapatia vijana jukwaa la kuonyesha vipaji vyao
na kujiweka sawa katika mchezo wa Soka. Kwa miaka 7 mfululizo tumekuwa
tukiendesha mashindano ya mpira kwa vijana kupitia program yetu ya Airtel
Rising Stars na leo tumeona ni vyema kuwafikia vijana mitaani kwa kudhamini
mashindano ya mpaira wa miguu katika ngazi ya wilaya ili kuwezesha vijana wengi
kuonyesha vipaji vyao na kutumiza ndoto zao”.
“Tunaushukuru uongozi wa mpira wa wilaya ya
kinondoni kwa kutualika kushiriki nao ni matumaini yetu kupitia mashindano haya
tutaweza kuwaunganisha vijana pamoja, kuchochea kukua kwa mpira wa soka nchini
lakini pia kuamashisha mashindano ya mitaani yaweze kufanyika na kuwa na mvuto
Zaidi huku vijana wengi Zaidi wakipata nafasi ya kushiriki.
Tunatoa wito kwa vijana na timu zilizojiandikisha
kutumia fursa hii vyema kwani mpira wa miguu ni ajira na njia ya kupata
kipato. Airtel tutaendelea kushirikiana na viongozi wa soka katika wilaya
mbalimbali nchini katika kuhakikisha tunatoa nafasi kwa vijana kushiriki
mashindano kama haya na kuwajenga Zaidi na kuwafanya wawe wanasoka bora ndani
na nje ya nchi.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa soka la vijana
wilaya ya Kinondoni, Abdallah Singano alisema “Tunawashukuru sana Airtel kwa
kukubali kudhamini mashindano haya kwa kutoa zawadi za washindi.
Ushiriki wa Airtel umeongeza mvuto wa mashindano
haya na mwitikio umekuwa mkubwa sana. Hadi sasa tunazo timu 64 ambazo
zimekwisha jiandikisha siku ya Jumamosi na Jumapili ili kushiriki mashindano
haya, usajiri huu ulifanyika katika viwanja vya KIFA Mburahati, Msasani CCM
magunia, Mwananyamala ETIHAD pamoja na uwanja wa Tegeta.
Timu zote ziko tayari na sisi kama wasimamizi
wakuu wa mashindano haya tumejipanga kusimamia vyema mashindano haya ili yaweze
kuendelea kuleta tija katika soka letu”
Napenda kutoa wito kwa wapenzi wa mpira mashabiki
kujitokeza kwa wingi kufatilia michuano hii pindi itakapoanza kutimua vumbi
hapo tarehe 8 octoba katika viwanja mbalimbali wilayani Kinondoni, ratiba
kamili ya mashindano hayo itatolewa pindi itakapokamilika”
Katika michuano hiyo Airtel imetoa zawadi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jezi, kombe, Soksi , shin guard, Tshirts,
medali, pamoja na zawadi mbalimblai kwa wachezaji bora wa michuano
hiyo. Jumla ya Zaidi hizo zina dhamani ya shilingi millioni tano.
Airtel supports youth tournament in Kinondoni district
Airtel Tanzania has donated sports gear to Kinondoni Football
Association (KIFA) which will be used during the U-17 Chipukizi tournament
scheduled to kick off on October 8 within the district.
The tournament which is expected to feature 64 teams is aimed to
give the youth an opportunity to showcase their talents and expose them to
coaches who will select a combine youth team for the district.
Speaking in Dar es Salaam during the event to handover the sports
gear, Airtel Tanzania Sales Manager for Dar es Salaam region Brighton Majwala
said ‘today is a special for us Airtel as we have decided to extend our reach
for the youth. As you are aware, Airtel Tanzania has been sponsoring the Airtel
Rising Stars for seven years and thus we have decided to sponsor youth teams
within district level so that we can have a reach to as many young footballers
as possible’.
We appreciate the Kinondoni Football Association (KIFA) for
welcoming us to support Chipukizi Cup and I’m sure through this competition we
will be able to bring the youth together, said Majwala.
I call upon the teams that have registered to participate the
tournament to make full use of the opportunity in order to excel. Airtel
Tanzania will continue partnering with other districts and regions in order to
make sure that youth football is recognized and supported, added Majwala.
We appreciate Airtel Tanzania for sponsoring this tournament.
Airtel presence has added a great happiness and the attendance has been
excellence. So far we have a total of 64 teams which have registered and we are
ready for kick off on October 8, said Kinondoni District Chairman of youth
tournament Abdallah Singano.
I call upon football fans to come up offer motivations to the
players during the tournament, added Singano.
In supporting the tournament, Airtel has donated Jerseys, socks,
shin guard, Tshirts, medals all worth Tzs 5 million.
No comments:
Post a Comment