Tangazo

Showing posts with label Miundombinu. Show all posts
Showing posts with label Miundombinu. Show all posts

May 25, 2018

RC DK. KEBWE AAGIZA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI GAIRO WAKAMATWE

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea maelezo ya wizi wa pampu ya maji kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe ili kuweza kuwalejeshea wanachi maji. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe  amesema nashangaa kuona pamoja na changamoto mliyonayo ya maji ila kuna watu bado wanahujumu miundo mbinu yenu jambo linakosesha majibu sahihi, walioiba Pampu hiyo ya maji hawajatoka nje ya kijiji cha Italagwe... naomba OCD ufanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini mwizi na pampu ipatikane mara moja.
Kisima kilichoibiwa pampu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakielekea kukagua mradi wa maji uliokuwa unasumbua.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakitoa pole kwa wafiwa wilayani katika kijiji cha Tabuhoteli -Gairo wakati wa ziara yake ya siku tatu anayoifanya ili kuchochea maendeleo shughuli za maendeleo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Tabuhoteli katika kata ya Chigela - Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa salamu zake kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakiongoza wananchi kuelekea katika mradi wa maji wa Ihenje.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakipokelewa kwa ngoma.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe wakimsikiliza Mhandisi wa wilaya ya Gairo, Heke Bulugu wakati akitoa maelezo ya 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe akitoa neno la shukrani.
Wananchi waliohudhuria.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Rachel Nyangasi akiwasalimia wananchi wa kata yake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wananchi.

March 27, 2018

DK. KALEMANI AWAPA MAAGIZO WAKANDARASI WA REA NCHINI


Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii ch a Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Y ona Mark na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuluni Selemani Omari
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akiteta jambo mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumban i Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akisalimiana na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji ni awamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na waataalamu mbalimbali wanaotekeleza mradi wa rea awamu ya tatu mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Sehemu ya wananchi wakifuatilia uzinduzi huo
Ssehemu ya wakandarasi wakifuatilia uzinduzi huo

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza wa wakala wa nishati vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye vijiji vitatu kila wiki ili kuweza kutoa fursa ya wananchi kufikiwa na huduma hiyo muhimu.

Dkt Kalemani aliyasema hayo leo wakati akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA III) katika kijiji cha Magumbani kitongoji cha Mbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga.

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na uwashwaji wa huduma ya umeme katika Kijiji hicho ili kuwawezesha kupata huduma hiyo ilikuwa haipo awali katika eneo hilo

Alisema kwani hayo ndio malengo waliowapa ikiwa ni mpango mkakati wa kuha kikisha wanafikia malengo ya kuwapelekea umeme watanzania wote ifikapo mwaka 2021/2022 ili waweze kunufaika kupitia huduma hiyo

“Leo tutaangalia mlipowasha lakini niwaagize wakandarasi tunataka kuona kila wiki vijiji vitatu vinawashwa umeme kwani wananchi wanauhitaji mkubwa wa kufikiwa na huduma hiyo hivyo hakikisheni hilo mnalitilia mkazo mkubwa “Alisema.

Hata hivyo alisema bado kuna changamoto ya wananchi kutapeliwa na mafundi ambao wamekuwa wakiwabambikia bei kuwaambia walipe kidogo kabla ya kulipia 27000 ambazo wanapaswa kulipa jambo ambalo ametaka likomeshwe haraka.

“Mameneja, Wakandarasi tuna changamoto wananchi kutapeliwa kuna tabia imezuka mafundi wanawabambikia bei wanaawaambia walipe kidogo kabla ya kulipa elfu 27000 labda niwaambie tu kwamba mtu wa namna hiyo atakayepatikana watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria”Alisema Waziri huyo.

Alisema mradi huo utakwenda kila kijiji, kitongoji na nyumba kwa nyumba huku akieleza hata kama nyumba unayokaa utaona hakuna sehemu ya kutundukia waya weka hata kwenye mti ili mradi uweze kufikiwa na huduma hiyo.

Aidha alisema kusudio lingine ambalo alilojia ni kuweka msukumo kwa wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana ili kuweza kumaliza mradi huo kwa wakati ili walengwa waweze kunufaika nao.

Waziri huyo pia aliwataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya umeme ikiwemo Transfoma kwa kuhakikisha kutokuiba mafuta kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ukuaji wa maendeleo.

“Ndugu zangu tukishirikiana kuilinda miudombinu ya umeme kwani serikali inatumia gharama kubwa kuifikisha kwenye maeneo yenu lakini pia Diwani wa Kata hii anzeni kutenga fedha kwa ajili ya kuunganisha kwenye taasisi za umma kwenye maeneo yenu”Alisema(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

February 27, 2018

AWESO AHAIDI NEEMA KWA WAKANDARASI WA MAJI WAAMINIFU

Na Mwandishi Wetu. Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi serikali kupitia wizara ya Maji kulipa kwa wakati wakandarasi waaminifu wanaosimamia miradi ya Maji ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu. Mheshimiwa Aweso ameyasema hayo Jijini Dar kwenye siku yake ya nne ya kikazi alipokuwa akikagua maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa na Manispaa pamoja na Miradi ya DAWASCO na DAWASA. "Wizara ya Maji inajitahidi kutengeneza miradi ya maji itakayomaliza tatizo la Maji kwa wananchi hususani wananchi wenye kipato cha chini hasa vijijini, hivyo mkandarasi atakayefanya kazi yake vizuri na kwa wakati sisi kama serikali hatutasita kumlipa kazi yake kwa wakati"alisema Aweso Katika ziara yake hiyo, Mheshimiwa Aweso alitembela miradi ya Maji ya Hondogo, Kibamba, Kingazi A pamoja na Mburahati.
Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akiangalia bomba lililopasuka.

February 8, 2018

TANESCO SUMBAWANGA YAPOKEA JENERETA YA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 10

  NA SAMIA CHANDE, SUMBAWANGA

KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta  ya kufua umeme yenye uwezo  wakuzalisha MegawatI 10 zitakazoimarisha uzalishaji wa umeme mkoani humo.
Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo, Meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Bw.Herini Muhina, alisema, hali ya uzalishaji umeme itakuwa bora zaidi na hivyo kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga, Laila, Kalambo na Nkasi kuwa bora zaidi.


“Nimatumaini yetu kuwa ongezeko hilo la umeme, litasaidia kwenda sambamba na mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kwani umeme wa uhakika utakuwepo na hivyo kufanya Mkoa wa Rukwa kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza kwenye sekta hiyo ya viwanda.” Alitoa hakikisho Bw. Muhidin.
Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali Watu wa TANESCO Makao Makuu, Bw. Nathan Daimon(wane kushoto), akipatiwa maelezo kuhusu jenereta hiyo na mdhibiti na mwendeshaji mifumo ya umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw.Halfan R. Seba
  Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali Watu wa TANESCO Makao Makuu, Bw. Nathan Daimon (watatu kushoto), akipta maelezo kutoka kwa mdhibiti na mwendeshaji mifumo ya umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw.Halfan R. Seba  kuhusu jenereta ujio wa jenereta yenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 10 kwenye kituo hicho.

Bw. Daimon akipewa maelezo zaidi ya uendeshaji shughuli za TANESCO mkoani Rukwa.
 

February 7, 2018

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WIZARA YA NISHATI MH.SUBIRA MGALU MKOANI KILIMANJARO

Tarehe 24 - 26/01/2018 Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya umeme vijijini (REA II & REA III) kwenye jumla ya vijiji 18 katika wilaya za ROMBO, MWANGA NA SAME Mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongea na wananchi, pia kutambulisha wakandarasi wa miradi ambapo aliwaagiza wakandarasi waepuke kurudia makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.

Pia Katika ziara hiyo Mh. Naibu waziri alitembelea bwawa la kuzalisha umeme la NYUMBA YA MUNGU kujionea shughuli za uzalishaji.

Mh Naibu waziri amemaliza ziara yake 26/01/2018 saa 12:00 jioni na kuelekea mkoani TANGA.

Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mkisha kuhusu kifaa kijulikanacho kama UMETA (REDY BODY) kifaa hicho hutumika kama mbadala wa kusuka mifumo ya waya (wiring) ndani ya nyumba. Aliyeshika kifaa hicho ni Afisa uhusiano TANESCO KILIMANJARO Bw. Samuel Mandari.

 Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasikiliza wanakijiji na kueleza uhitaji wa huduma ya umeme.

Wanakijiji wakimsikiliza Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) akieleza uhitaji wa huduma ya umeme.


Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa wilaya ya Same Mh. Rosemary Senyamule, Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, wakiwa na viongozi wa TANESCO MKOA wa Kilimanjaro walipo tembelea Kijiji cha Vunta wilayani Same.