Dk. Chrisant Mzindakaya |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Chrisant Mzindakaya kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa- NDC.
Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Viwanda na Biashara na kusainiwa na Katibu Mkuu Bi Joyce Mapunjo, imesema kuwa uteuzi huo umeanza tangu Julai 8,2011.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami amewateua wajumbe wengine tia wa Bodi hiyo.
Wajumbe walioteuliwa ni Prof Idris Kikula ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Makenya Maboko (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na Prof. Ntengua Mdoe (Mhadhiri Mwandamizi, chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine).
Wajumbe wengine walioteuliwa katika bodi hiyo ni Dkt Marcelina Chijoriga, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana Gabriel Masenga (Mkemia wa kampuni ya Far Chemical and Traveling Agency), Prof Abdulkarim Mruma (Giorogical Survey of Tanzania) na Bi Sondo (Wakili wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania).
Wengine ni Bi Eline Sikazwe (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Bwana Gideo Nassari ambaye ni Mkurugenzi wa NDC.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo utadumu kwa muda wa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment