Tangazo

August 16, 2011

Ofisa wa Benki afumaniwa Sinza

Mjumbe wa nyumba kumi Sinza B, Ruth Manfred (71) akiandika jina na saini yake kwenye karatasi ambalo wajumbe waliohudhuria kusuluhisha fumanizi hilo waliandika majina yao na kutia saini kumaliza mzozo. Kushoto ni mmoja wa wajumbe hao akimmulikia  kwa tochi ya simu.

NA MWANDISHI WETU

Mwanamke mmoja Ofisa wa benki moja hapa nchini, amelazimika kujifungia chumbani kwa zaidi ya saa nne, kunusuru maisha yake baada ya kufumaniwa katika chumba cha mume wa mtu mjini Dar es Salaam.

Tukio hilo ambalo lilikusanya kundi la watu, lilitokea  mwishoni mwawiki iliyopita  nyumbani kwa mkazi wa eneo la Sinza E,aliyetajwa kwa jina la Godfrey Iriya ambaye ni mfanyabiashara maarufu katika viunga vya Kariakoo jijini.

Ofisa huyo wa benki alijifungua chumbani, tangu saa 11 jioni hadi saa nne usiku, mwanamke anayedai kumfumania mwenzake, alipoamua kuondoka baada ya mjumbe wa shina na Mwenyekiti wa Mtaa na majirani kadhaa kusuluhisha.

Kiasi cha saa 11 jioni, Joyce Augustine ambaye inadaiwa ndiye mke halali wa Iriyo alifika kwenye nyumba hiyo baada ya kuwa kwao mkoani Rukwa tangu mwaka jana baada ya kutokea mzozo kati yake na mumewe.

Akisimulia tukio tukio, hilo mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo, alisema, Joyce alifika muda mfupi baada ya Ofisa huyo wa benki kuwasili akitokea kazini.

Alisema, ofisa huyo akiwa ameshaingia ndani, Joyce alienda moja kwa moja kwenye chumba alimokuwa akiishi na mumewe lakini hakufanikiwa baada ya kukuta mlango umefungwa kwa ndani.

Alijaribu kupiga hodi lakini aliyekuwa ndani hakujibu lolote wala kufungua mlango, ndipo Joyce akaenda kuita mjumbe wa nyumba kumi, ambaye alifika na kufajaribu pia kugonga mlango pia bila mafanikio.

"Wewe mtu uliyeko ndani, mimi ni Ruth Manfred, mjumbe wa nyumba kumi mtaa wa Sinza E, tafadhali fungua mlango kuna shida hapa..." aliita mjumbe huyo zaidi ya mara tatu akipaza sauti lakini bila mafanikio.

Baadaye alifika Mwenyekiti wa mtaa Kasim Kaburu, naye hakufanikiwa, ikabidi aite wazee na baadhi ya watu wa makamo kuja kusaidia mkasa huo.

Walipofika ikatafutwa njia itakayowaridhisha wao na mfumaniaji kwamba kweli kulikuwa na mtu ndani na mtu mwenyewe ni mwanamke.

Aliitwa mtoto Jacqueline Godfrey (13), ambaye anayeishi katika nyumba hiyo na alipoulizwa ikiwa anafahamu lolote kuhusu mtu aliyepo chumbani, alijibu "Ndiyo huyo, mwanamke ambaye baba anasema niwe namuita Anti, ametoka kazini akazingia humo, chumbani hadi sasa", alisema mtoto huyo wa kike ambaye jina tunalihifadhi.

Baada ya tamko la mtoto huyo, wazee na wajumbe wengine wa kikao cha ghafla, walishikwa na butwaa wakitazamana, "Mmesikia jamani, ni kweli kuna mwanamke humu ndani, huyu mtoto hawezi kuongopa, lakini sheria bado haituruhusu kuvunja mlango maana baba mwenye nyumba hayupo", walisema.

Ili kumtuliza aliyefumania, ikabidhi yaandikwe maelezo kuthibitisha kwamba Joyce amefika na amekuta kuna mwanamke ndani kulingana na ushahidi wa yule mtoto baadae Mwenyekiti wa Mtaa, mjumbe na walioshuhudia wote waliandika majina na kutia saini katika katarasi ya maelezo hayo.

Akielezea tukio hilo, Joyce alisema, ameamua kurejea na kufanya fumanizi kwa sababu baada ya kuzozana na mumewe aliondoka kwenye nyumbai kwao Rukwa, lakini baadaye mwanamume alifuata huko na kuitisha baraza akilalamika kwamba anamtaka mkewe huyo na hajaamuacha.

"Nikamuuliza kama hujaniacha mbona najua kwamba una mwanamke ofisa wa benki... unaishi naye kimada nyumbani? akanijibu hapana sina mwanamke." alisema Joyce nakuongeza " lakini nimeshangaa leo nilipofika hapa nyumbani, nimetaka kuingia chumbani kwangu nikaona mwaname anaingiachumbani humo humo na kujifungia". Story kwa hisani ya Nkoromo Daily Blog

No comments: