Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akiwasiliana na Padri Andreas Isaya Gowa mara baada ya kuchezesha Droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masoko wa Airtel, Alice Paulsen na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Milao . PICHA/DAILY MITIKASI BLOG Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, imempata mshindi wa milioni 50/- na kuongeza muda wa promiosheni hiyo kwa kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani huku ikiwa imewazawadia wateja wake jumla ya milioni 305/- hadi kufikia jana.
"Leo tunampatia mshindi mkuu wa promosheni ya Kwanjuka kwa kipengele cha kwanza na pia tunaongeza muda wa promosheni pamoja na zawadi ambapo kuanzia sasa washindi watajishindia 1,000,000/- kila siku na 5,000,000/- mwishoni mwa wiki wakati katika kilele mshindi kwenye droo kubwa ataondoka na milioni 20/- pesa taslim". alisema Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando.
Promosheni ya Kwanjuka imeongezewa muda wa siku 31 na itahusisha wateja wote wa Airtel Tanzania watakaoshiriki na ili kushiriki mteja anatakiwa kutuma neno KWANJUKA kwenda namba 15656 kisha mteja atapata maswali na akiyajibu kwa usahihi atajiongezea pointi za kuwa mshindi.
Aidha alifafanua kuwa leo ilikuwa ndio kilele cha promosheni hiyo tangu ilipoanza Aprili 2011 ,lakini kutokana na faida nzuri waliyoipata na wateja kuipenda sana promosheni hiyo basi wameamua kuongeza zawadi pamoja muda wa wateja kushiriki promosheni hiyo.
Kufuatia droo hiyo Padri Andew Isaya Gowa wa Parokia ya Mofu Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge mkoani Morogoro aliibuka mshindi wa milioni 50/.
Aidha Meneja wa Bidhaa na Mawasiliano, Rahma Mwapachu aliongeza kwa kusema, Airtel inawahimiza wateja kuendelea kushiriki katika shindano hilo ambalo limeongezwa muda wake na linaendelea ili kupata nafasi za kujishindia zaidi zawadi mbalimbali zilizoko.
"Tunafuraha kuwajulisha kuwa promosheni hii imekuwa ya mafanikio na washindi wamepatikana kutoka sehemu mbalimbali nchini huku ikiinua maisha yao jambo ambalo ndio lengo halisi la promosheni hii". alisema Mwapachu.
Aidha alimalizia kwa kusema kuwa kampuni yake inawaahidi watanzania kuendelea kupanua mtandao wake zaidi ili uweze kuwafikia wanainchi wote hasa wale waishio vijijini kote nchini ambapo Mwezi uliopita ilizindua huduma zake kwenye zaidi ya miji na vijiji 50 ikiwa ni katika kutimiza lengo la kuwafikia watu wengi na kuinua kiwango cha maisha yao na nchi nzima kwa ujumla.
|
No comments:
Post a Comment