Tangazo

August 25, 2011

RAIS KIKWETE AZIMA NDEREMO, VIFIJO WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, David Jairo
SIKU moja tu baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, kutangaza kumrudisha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo kwa kile kilichoelezwa kuwa hakupatikana na hatia, leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza rasmi kumsimamisha tena kazi katibu huyo Jairo, ili kupisha uchunguzi wa Tume iliyoombwa na wabunge kuundwa ili kuchunguza kwa umakini undani wa tuhuma zilizotolewa na Wabunge dhidi ya Katibu huyo.

Baada ya kutangazwa kurejeshwa kazini kwa katibu huyo, Wabunge walihoji uhuru wa mhimili wa Bunge na kuingiliwa katika maamuzi yake jambo lililozua mjadala na wabunge hao kutoa hoja bungeni ya kuundwa kwa Tume ya uchunguzi juu ya jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuchunguza mambo mengine.

Furaha ya Jairo imedumu kwa masaa kadhaa tu baada ya kupokelewa kwa shangwe na ndelemo wakati alipowasili kuripoti ofisini kwake jana huku baadhi ya wafanyakazi wakimlazimisha kuzima gari lake na wao wakaanza kazi ya kulisukuma hadli mahala pa maegesho, huku waziri wake akifurahi kwa kurejea kwa Katibu huyo wizarani hapo ambapo alisema kuwa nashukuru Sheria imefuata mkondo wake kwa kutenda haki kwa Katibu huyo.

No comments: