Chumo, mojawapo ya filamu za Tanzania zilizofanikiwa katika soko la kimataifa kwa sababu ya kuwezeshwa na taasisi za Kiserikali na za kifedha. WIKI iliyopita nilianzisha mjadala kwa njia ya swali: “upi mfumo unaotufaa kwa ajili ya filamu zetu?”, katika mjadala huu wasomaji kadhaa wamejitokeza kuchangia mawazo yao, ingawa wengi wao wameonekana kukubaliana na hoja nilizotoa kwa asilimia mia jambo ambalo sikubaliani nalo na sikuwa nikilihitaji. Naomba ieleweke kuwa yale niliyoyaandika ulikuwa ni mtazamo wangu binafsi ambao sidhani kama unaweza kuwa sahihi kwa asilimia mia kwa mia, kuanzisha mjadala kulikuwa na maana ya kutaka kupata hoja kinzani na mawazo mbadala yanayoweza kusaidia kuboresha soko letu. Sikuanzisha mjadala ili nisifiwe na kujaziwa pongezi kemkem. Kati ya wasomaji wote walionitumia ujumbe na wengine kunipigia simu ni msomaji mmoja tu ambaye angalau alikwenda mbali zaidi akijaribu kuzitazama fursa za masoko ya filamu zetu si ndani ya nchi tu bali hata nje ya nchi. Siku za hivi karibuni uzalishaji kwa kutumia kazi za sanaa nchini, hususani filamu, umekuwa ukichukuliwa kama kimbilio kwa wasiojiweza au walioshindwa katika fani zingine kama njia ya kujikwamua kiuchumi na kuendeleza utamaduni.source:www.bishophiluka.blogspot.com |
August 5, 2011
Zipi fursa za masoko ya filamu zetu nje ya nchi?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment