Tangazo

September 29, 2011

AIRTEL YACHANGIA ZAIDI YA MILLION 40 WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Airtel kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma zenye gharama nafuu na za uhakika ya jana imechangia  juhudi za serikali kupitia jeshi la polisi usalama barabarani zaidi ya kiasi cha million 40 katika kufanikisha na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usalama barabarani  lengo likiwa ni kuthibiti na kupunguza idadi ya ajali za barabarani.

Airtel imetoa vifaa mbalimbali kwa jeshi la polisi ikiwemo kuchapisha sticker za kuthibitisha ukaguzi wa magari nchini, katika vifaa hivyo zimo Tshirt 2200 zenye ujumbe wa usalama barabarani kwa mwaka huu usemao” Usalama Barabarani unahitaji juhudi za kila moja wetu”  vile vile Airtel imetoa kutoa namba za simu  kwa kituo chetu cha mawasiliano (Kazimoja Information Centre). Vifaa vyote vina dhamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 .

Akiongea kwa niaba ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano Bi Beatrice Singano Mallya alisema, “Airtel inatambua jukumu tulilonalo katika kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa,  kwa miaka mitatu mfululizo sasa Airtel imekuwa ikishirikiana na jeshi la polisi katika kufanikisha zoezi la usalama barabarani,sisi kama watanzania tunatakiwa tuzingatie sheria,tushirikiane na vyombo husika kutoa taarifa zinazo hatarisha usalama wa barabarani.Tusijiulize polisi wa usalama barabarani wanafanya nini ila tutoe taarifa pale tunapoona sheria zinakiukwa.Mwaka huu vibandiko vyote vina namba za simu,rai yetu kwa watanzania ni tuongeze juhudi kufichua uovu unaoweza kuleta madhara barabarani” .

Sisi kama kampuni ya mawasilaino ya Airtel tu nayofuraha kuchangia na kuwa sehemu ya jitihada za kuokoa  maisha ya watu katika jamii yetu.lLengo hasa likiwa ni kuhakikisha ajali za barabarani zinathibitiwa na kupungua kwa kasi zaidi kuliko ilivyo tarajiwa. Sambamba na hili tunajitoa ili kuweza kuhamasisha jamii nzima kuzingatia usalama barabarani  kwani adha za ajali za barabarani kukubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla na zinapunguza nguvu za uzalishaji.

Tunahaidi kuendelea kushirikiana na baraza la taifa la  usalama barabarani,jeshi la polisi na taassisi husika katika kuhakikisha usalama wa raia na maisha yao unatiliwa mkazo na kuzingatiwa na waendeshaji na wamiliki wa vyombo vya moto.

 Akiongea wakati wa kupokea msaada huo kamanda wa polisi Mohamed Mpinga alisema, “Tunaishukuru sana kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa juhudi zao na kwa kutuunga mkono kila mwaka katika zoezi hili nyeti la kitaifa, Kuanzia tarehe leo tarehe 28/09/2011 BARAZA la Taifa la Usalama Barabarani kupitia Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani nchini limeanza rasmi zoezi la ukaguzi wa magari yote  Nchi nzima kama inavyofanyika kila mwaka wakati wa wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
 
Lengo la ukaguzi huu ni kuhakikisha magari yote hapa nchini yanakaguliwa ili kuyabaini yale mazima yaendelee kuteambea barabarani na yale yaliyokithiri kwa ubovu kuondolewa barabarani ili kudhibiti ajali za barabarani zinazotakana na ubovu wa magari.

Mwaka huu Sticker hizi za ukaguzi zimetofautiana kwa aina na  Ada inayotozwa, ambapo kuna sticker kwa ajili ya magari ya binafsi [Private Vehicles] ambazo ni Tshs 3,000/=  kwa ajili ya magari ya biashara [Commercial Vehicles] ni Tshs 5,000/= na pikipiki, Bajaj ni 1000/=. Sticker(vibandiko) hivi vitaanza kutolewa tarehe 28/9/2011 na vitapatikana katika sehemu zifuatazo Ilala  - Trafic ilala – msimbazi, karume, Buguruni, stakishari.  Kinondoni – Oysterbay, Magomeni, ubungo, Mbezi kwa Yusufu, Mwenge, Kawe na Tegeta wakati Temeke – changombe, mbagala, kigamboni, Tandika

Tunapenda kuwatahadharisha wananchi wote wanaomiliki magari kwamba zoezi hili la ukaguzi wa magari ni la lazima na hawatakiwi kwenda kununua sticker hizo kwa njia za ujanja ujanja, wanachotakiwa ni kuyapeleka magari yao kukaguliwa na gari lisilo na dosari ndilo litapata sticker ya ukaguzi ya BARAZA la Taifa la Usalama Barabarani.

No comments: