Tangazo

November 16, 2011

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZIDI KUWAHAMASISHA WATANZANIA KUHUSU TUSKER CHALLENGE CUP

Kampuni ya bia ya Serengeti wakishirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Africa Mashariki na Kati (CECAFA) imetangaza rasmi ratiba ya michuano ya kuwania kombe la Tusker maarufu kama’ CECAFA Tusker Challenge Cup 2011’ inayotarajia kutimua vumbi kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10 hapa nchini Tanzania . Maandalizi yashakamilika.

Katibu mkuu wa Shirikisho mla Mpira wa Miguu nchini TFF Angetile Osiah alitangaza rasmi ratiba hiyo ya makundi katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti na kufanyika katika ofisi za TFF Karume jijini Dar es Salaam leo.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na ujumbe kutoka TFFukiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Leodger Tenga, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Ephraim Mafuru na Meneja wa bia yaTusker Bi. Rita Mchaki.

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake yaTusker ni mdhamini mkuu wa michuano hiyo ambapo imetoa kiasi cha Shilingi milioni 823. Takribani timu 11 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo zikiwemo timu ya Malawi ambayo itacheza kwa mwaliko maalum.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya bia ya serengeti,Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru amesema muhimu watanzania watambue heshima iliyopewa Tanzania na shirikisho la mpira wa mguu kuwa wenyeji wa mashindano ya CECAFA na walichukulie jambo hili kibinafsi kabisa wajitokeze kwa wingi katika michuano yote kama ratiba inavyoelekeza. ’Mimi naomba watanzania wote tujitokeze kwa wingi tushangilie timu zetu,’ alikaririwa Bw. Mafuru

Ephraim Mafuru amewataka watanzania wote kwa ujumla kuja kwa wingi na wawe tayari kuburudika, kwani kupitia bia ya Tusker, mechi za CECAFA mwaka huu zitakuwa na msisimko wa aina yake,’ zawadi kem kem zitashindaniwa kupitia kinywaji bora cha Tusker.

Ephraim Mafuru ameomba makampuni mbalimbali kuitokeza na kushirikiana na SECAFA pamoja na Serengeti katika kudhamini mashindano hayo na wao kama Kampuni ya bia ya Serengeti wako tayari kushirikiana kwa manufaa ya mpira wa nchi yetu Tanzania.

Mashindano hayo sasa hayatafanyika Mkoani Mwanza kama ilivyokuwa imekusudiwa hapo mwanzo badala yake michezo yote itachezwa jijini Dar es salaam katika uwanja wa Taifa na Chamazi katika uwanja wa Azam.

Mwaka huu, timu zitakazoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Djibouti, Somalia, Ethiopia, Sudan, Tanzania, Zanzibar, ambapo timu ya Eritrea imejitoa na timu zilizoalikwa kushirikia mashindano hayo ni Malawi na Namibia.

Kampuni ya bia ya Serengeti inapata heshima ya kuwa mdhamini mkuu na kupata haki miliki ya kutumia nafasi hii kutangaza bidhaa yaTusker kipindi chote cha mashindano haya.

No comments: