Tangazo

February 22, 2012

Mheshimiwa 'Sugu' na Ruge sasa 'Damu Damu'

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba  wakipeana mikono  jijini Dar es Salaam Februari 21.12, ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa  tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusiana na  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu  kwa muda wa miaka miwili.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi  akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia).

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu  kwa muda wa miaka miwili.

No comments: