Tangazo

February 22, 2012

Wateja 700 wa M-PESA wajazwa Manoti

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza
Wateja 700 wa Vodacom MPESA wamejishindia kiasi cha shilingi 35 Milioni katika wiki ya kwanza ya promosheni ya tuma fedha kwa MPESA na ushinde ilyozinduliwa wiki iliyopita ambapo jumla ya Shilingi 480 milioni kushindaniwa.

Washindi hao ambao kila mmoja amejishindia kiasi cha shilingi 50,000 katika droo za kila siku. Mbali na droo ya kila siku promosheni hiyo itachezesha droo moja kubwa kw akila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu zitakazotoa washindi wa Shilingi 10 Milioni kila mmoja.

“Hadi kufikia leo promosheni hii imeshatoa washindi mia saba, haya ni matokeo ya mwitikio mzuri wa wateja wetu kushiriki na hii inatupa faraja kwetumkwa kuwa lengo la Vodacom ni kuwafanya wateja wetu kuwa na furaha watumiapo huduma yetu ya MPESA na kuwawezesha.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza

Kupitia droo hiyo washindi mia moja hujishindia shilingi 50,000 kila mmoja ambazo mshindi huingiziwa moja kwa moja katika akunti yake ya MPESA.
.
Mwamavita amesema huduma ya MPESA imekuwa sehemu muhimu katika maisha ya wananchi ambayo imerahisha na kubadili maisha yao tangu ilipoanzishwa Aprili, 2008, na hii inaenda sambamba na azma ya Vodacom ya kuthamini mchango wa wateja wake kuunga mkono huduma hiyo kwa kuwawezesha na pia kuifanya kuzidi kuwa huduma bora,salama,ya uhakika na rahisi..
 
“Ni msimu mwengine ambapo tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufurahia huduma bora,rahisi,salama na ya kuaminika ya Vodacom MPESA kwa gharama nafuu zaidi sokoni kutoka kampuni inayoongoza soko la huduma za simu za mkononi nchini. Alisema Bw. Rene katika taarifa yake kwa vyombo vya habari..

“Matumizi ya huduma ya Vodacom MPESA yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana, na hii inatufanya wakati wote kuongeza kasi ya kuifanya huduma ya MPESA kuendelea kuwa huduma bora zaidi sokoni na yenye tija kwa wateja wetu inayotoa huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi. Kadri mteja anavyotuma pesa kwenda kwa mteja wa MPESA aliyesajiliwa au ambae hakusajiliwa ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya juu ya kushinda zawadi katika promosheni hii”Aliongeza Bw. Rene

Huduma ya Vodacom MPESA ina mtandao wa mawakala zaidi ya elfu kumi na tano nchi nzima na wateja zaidi ya milioni nane kati yao zaidi ya milioni mbili wakifanya miamala – kutuma na kupokea fedha kwa kipindi cha mwezi mzima mfululizo.

Kupitia huduma ya MPESA mteja wa Vodacom aliyejisajili na huduma hiyo anaweza kufanya manunuzi ama kulipia huduma mbalimbali za ikiwemo umeme – LUKU, DAWASCO,DSTV,Muda wa maongezi, kuchangia michango ya harusi,kusaidia misiba, ada, n.k ndani ya nchi na hata kutokea nje ya nchi.

Mbali na promosheni hii wateja wa MPESA kwa sasa wanafurahia pia ofa mbalimbali ikiwemo ya punguzo la asilimia 75 katika gharama za kutuma fedha kwa MPESA mabapo sas amteja anatuma fedha kwa kiwango cha chini kabisa cha shilingi 50 kuanzia shilingi 500 hadi elfu kumi, nyongeza ya bonasi ya asilimia 25 mteja anaponunua muda wa maongezi wa hewani kupitia MPESA.

No comments: