Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.
Kambi hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo februari 29, itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha Elimu Kibaha. Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya mbogamboga wilayani Rufiji.
Rais Kikwete ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi hizo na kutaka mikoa mingine iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa kuweza kujiajiri wenyewe.
Ameahidi kuendelea kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja kama hazina nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la ajira.
Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu.
Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake. PICHA NA HABARI/ IKULU |
No comments:
Post a Comment