Tangazo

March 15, 2012

KIMD Constructor yaanza Ujenzi wa Daraja la ITEBA jijini Dar es Salaam

Watoto washule wakipita katika daraja la muda lililowekwa na vijana wa Manzese katika Mto Iteba unaotenganisha Sinza na Manzese jijini Dar es Salaam. Pem,beni ni ujenzi wa daraja la kudumu ulioanza kufanyika hivi karibuni chini ya Kampuni ya Ujenzi ya KIMD kutoka Kibaha mkoani Pwani.

Meneja Miradi wa KIMD Constructor, Onesmo Nathan akielezea jambo kuhusiana na ujenzi wa daraja la watembea kwa Mguu la ITEBA linalounganisha Sinza na Manzese jijini Dar es Salaam linalojengwa na kampuni hiyo KIMD kutoka Mjini Kibaha mkoani Pwani. KIMD ni moja ya kampuni chache za Ujenzi zinazomilikiwa na wazawa kwa 100% na imekuwa ikifanya kazi nyingi za ujenzi wa barabara, mashule, na vituo vya afya katika maeneo mengi hasa Mkoani Pwani.

Wananchi wakipita katika daraja hilo la muda ambapo hutozwa fedha na vijana hao.

Muuza gahawa nae akipita jirani na eneo hilo la ujenzi wa daraja jipya ambalo linajengwa kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Kwamujibu wa Meneja Miradi wa KIMD, Onesmo Nathan  anasema ujenzi wa daraja hilo unataraji kuchukua majuma manne lakini pia itatokana na hali ya hewa itakavyo kuwa maana eneo hilo hujaa maji mengi wakati wa mafuriko.

No comments: