Usa River
Mbunge wa Korogwe Vijiji (CCM) Stephen Ngonyani 'Prof. Maji Marefu' (pichani),amedai kuwa leo asubuhi ameponea chupuchupu kuuawa baada ya mgombea wa CHADEMA jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuwaamuru vijana wa chama hicho wamchome moto, kisa amekanyaga eneo la gesti walimoweka kambi jimboni humo.
Taarifa zilizoufikia mtandao huu, zimesema Ngonyani aka Maji Marefu (pichani) amenusurika kutwishwa 'msalaba' huo kwa kuokolewa na waandishi wa habari walioingilia kati baada ya kudaiwa kusikia Nassari akitoa amri ya kikatili ya "mchomeni moto huyo".

Akizungumza na mwanamtandao wetu aliyeko Arumemeru Mashariki, Majimarefu amedai akiwa eneo la hoteli ya Elephant ambako CHADEMA imeweka kambi kwa ajili ya uchaguzi mdogo jimboni humo, aliwaona Mbunge wa Musoma Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Vicvent Nyerere na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHAEMA Taifa, John Heche, anasalimiana nao raha mustarehe.
Kisha akatokea alitokea Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa naye pia akasalimiana naye kwa bashasha kisha wakataniana, kwa wabunge hao kumbwambia Majimarefu "hapa ushindi ni CHADEMA" tu, naye akiwajibu kwa tabasamu " sawa tutaona nani mshindi baada ya kura kupigwa na wananchi Aprili mosi".
Majimarefu akasema, akiwa anaendelea ku-chati na wabunge wenzake na Heche aliona kundi la waandishi wa habari akaenda kusalimiana nao, ghafla alikatokea Nssari na kumuuliza amefuata nini pale.
"nikamuuliza kwani hapa kuna masharti ya kukaa watu, Nassari akaamrisha kundi la watu akisema huyu achomwe moto", akasema Majimarefu.
Alisema, baada ya kutamka neno nichomwe moto waandishi wa habari waliokuwa pale wakaingilia kati na kuniokoa, kisha na Heche na Nyerere na Msigwa nao wakaingilia kati kumuokoa.
Majimarefu akasema akiwa katika harakati za kujiokoa alipanda haraka teksi aliyokuwa amekuja nayo hapo, lakini hata baada ya kupanda, kundi la vijana lilijaribu kulikimbiza likiwa kwenye mwendo kwa lengo kulichoma moto.
Kwa mujibu wa ripota wetu, hadi anatuletea dondoo hii, Majimarefu alikuwa bado hajaripoti tukio hilo polisi, na inadaiwa mratibu wa Kampueni za Chadema Vincent Nyerere alikuwa akihaha kumpigia simu ili kum-plz asiende polisi.
"Unajua hawa watu watapeleka nchi pabaya, inakuwaje hadi mgombea mwenyewe anayetafuta kuwa kiongozi na nembo ya watu katika jimbo, aamrishe wazi wazi watu kuua? hii hali lazima Watanzania tuikatae mapema", alisema Majimarefu.
Habari kwa hisani ya Nkoromo Daily Blog

No comments:
Post a Comment