*****************
Na Ali Meja - OMR
Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF umetumia jumla ya shilling bilioni 5/- kisiwani pemba tokea mwaka 2006 katika miradi mbali mbali ya maendeleo.
Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF umetumia jumla ya shilling bilioni 5/- kisiwani pemba tokea mwaka 2006 katika miradi mbali mbali ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na maratibu wa mfuko wa TASAF pemba bwana ISA JUMA ALI alipokuwa akitoa maelezowa waziri wa nchi ofisi ya makamo wa rais muungano mh Samia Suluhu hasani katika ziara maalumu kisiwani pemba katika kukagua miradi mbambali ya maendeleo.
Waziri Samia yupo kisiwani pemba kwa zira ya siku tano kujioneshughuli mbali mbali za maendeleo ktika maeneo mbali mbali.
Akitoa mchanaganuoa wa matumizi ya miradi ya TASAF unaofadhili wa na serikali ya jamuhuri ya muungano , amesema kuwa katika maradi huo awamu ya pili wamefanikiwa zaidi ya miradi 347 imepataufadhili wa jumla ya shilling 5,544,696,611.
Miongoni mwa miradi ambayo imetembewa jana ni pamoja na mradi wa ufugaji nyuki kibokoni ambao umefadhiliwa jumla ya shilling million kumi hadi sasa .
Pia takatika zira hiyo mradi wa umwagiliaji maji wa DOBI WAWI ambao umepatiwa ufadhili wa jumla ya milon 39,947,710, ambao utwanufaisha jumla ya wananchi elfu mbili utakapo malizika .
Katika ziara hiyo mradi wa ujenzi wa barabara ya machomane ndugunkitu kupitia mkoroshoni mbao naopia umejegwa kwa hisani ya mfukowa maendeleo ya jamii wametakiwa kuwa makini na utunza wa miradi huyo ambao kipindi hiki cha mvua huwa ni matatizo makubwa hasa kwa mkukos misimamizi na kusababisha haribika haraka .
Wakati wa machana mh waziri wa nchi ofisi ya rais muungano alitmbelea katika soko la samaki liliopo wesha katika wilaya ya chake chake na kuwataka walengwa wa mradi huo kudhamini vizuri sana .
Nae kwa upande wake sheha wa shehia hiyo amemwahidi mh Samia kuwa hii ndio nafsi pekee kwao kujikomboa hivyo watalitunza soko hilo kama mboni ya jicho lao .
Aidha waziri huyo wa muungano yupo kiswani pemba kwa ziara za siku tano katika mikoa miwili pemba ambapo atatembelea miradi mbali mbali katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa na serikali inatoa faida kubwa sana kwa maslahi ya wananchi kwa umjumla .
No comments:
Post a Comment