Tangazo

March 12, 2012

Umoja wa Ulaya 'waipiga jeki' Tanzania Bilioni 108

Naibu  Katibu  Mkuu wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile akibadilishana hati za makubaliano  na Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya Filiberto Cerian Sebregondi katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 108 zimetolewa na umoja huo fedha ambazo zitatumika  kuimarisha  miradi ya maji katika mikoa ya Rukwa, Lindi na Kigoma ili kutimiza malengo ya milinia ifikapo mwaka 2015.

Naibu  Katibu  Mkuu wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile na Balozi wa nchi za Umoja wa Ulaya Filiberto Cerian Sebregondi wakisaini hati za makubaliano  katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 108 zimetolewa na umoja huo fedha ambazo zitatumika  kuimarisha  miradi ya maji katika mikoa ya Rukwa, Lindi na Kigoma ili kutimiza malengo ya milinia ifikapo mwaka 2015. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments: