Tangazo

March 13, 2012

Ujumbe wa IMF & Gavana Ndulu wazungumza na Waandishi wa Habari

Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu akijibu maswali ya waandishi wa habari  (hawapo pichani) mara baada ya Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum (kushoto) kumaliza kuongea na waandishi wa habari kuhusu uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.

Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum akiongea na waandishi wa habari  jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishwa na ukame mwaka 2011. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndulu.

Baadhi ya wajumbe kutoka  Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika wakifuatilia kwa makini mkutano huo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments: