Tangazo

March 21, 2012

Wafanyabiashara waulalamikia Uongozi wa Soko la Mchikichini jiji Dar

Mwenyekiti wa Tume wa Ufuatiliaji tatizo la Umeme katika Soko la Mchikichini,  Mussa Kitakuru Kweka (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Wanaharakati wa Soko la Mchikichini, Godwin Kaison Ndabazi na Mfanyabiashara wa Mchikichini,  Zabibu Ally Lukuba. Wafanyabiashara hao wamemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwapatia eneo la wafanyabiashara ndogo ndogo katika Soko hilo  na limeweza kuwapatia ajira ya zaidi watu 10,000 aidha Soko hilo limekosa umeme kuanzia Disemba 13/2011 hadi leo kutokana na kutolipa deni la  Milioni 230/- ambalo wamedai limesababishwa na Uongozi wa soko hilo. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Mwenyekiti wa Wanaharakati wa soko la Mchikichini Godwin Kaison Ndabazi (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 21.12,  kuhusu matatizo yanayowakabili  ya kukosa umeme pamoja na matatizo ya viongozi wa soko la Mchikichini  katika Manispaa Ilala .  Kulia ni Mwenyekiti wa Tume wa Ufuatiliaji tatizo la Umeme  Sokoni hapo, Mussa Kitakuru Kweka. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

No comments: