Tangazo

April 17, 2012

Tanzania Breweries Limited (TBL) yatoa Milioni 100/- kusaidia Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar

Baadhi ya wakufunzi na wafanyakazi wa chuo hicho wakifurahia msaada huo.

Mkuu wa Kikuu cha Tumaini, Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa,  Profesa Geoffrey Mmari (katikati) akielezea mikakati ya ujenzi wa majengo mapya ya chuo hicho. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo ambayo imetoa msaada wa sh. milioni 100 za kusaidia ujenzi wa majengo hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ushauri wa ujenzi wa majengo hayo, Nosuto Associated, Thomas Kalugula akielezea jinsi ujenzi wa majengo hayo utakavyofanyika.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto),akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Huduma za Jamii wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Robert Charles (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 100 za kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam. Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ni Mkuu wa chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Geofrey Mmari.

Naibu Katibu Mkuu Huduma za Jamii wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Robert Charles (kulia) akimshukuru Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 100 za kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Geoffrey Mmari.


Michoro ya majengo mbalimbali ya chuo hicho yatakayojengwa eneo la Mwenge, Dar es Salaam.

No comments: