Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu, Esther Kitoka. |
Meneja wa Huduma kwa Wateja, Godwin Semunyu. |
Baadhi ya Maofisa wa Benki hiyo. |
Dar es Salaam
IMEELEZWA kuwa tatizo la mfumko wa bei unachangia na kuathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya kifedha kwa kusababisha kupanda kwa gharama na kupunguza thamani ya fedha kwa kiasi cha asilimia 20.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika mkutano uliohusu matokeo ya kibiashara katika kipindi cha kwanza cha machi, mwaka huu ya benki ya CRDB, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk, Charles Kimei, alisema kuwa hatua hiyo inalazimu kutoa riba kubwa kwa wale wanaowekeza katika benki.
Dk, Kimei alisema kuwa baadhi ya wanaowekeza watashindwa kulipa riba hizo na kupelekea kuwa na ujazo mdogo katika soko la benki na kupanda kwa dhamana za kiserikali.
“Riba sasa katika soko la fedha linafikia asilimia 25…kwa kweli hali hiyo sio nzuri kwani hata wateja wa mikopo hawataweza kulipa ingawa kwa upande wetu hadi sasa bado hatujaongeza riba kwani tunatarajia hali ya soko kushuka,” alisema.
Dk. Kimei, alisema kuwa sehemu kubwa ya mfumko wa bei ni kutokana na vyakula kuuzwa kwa bei hasa vinavyotoka nchini hatua iliyochangiwa na ukosefu wa hali ya mvua wakati wa kilimo.
“Hatuna budi kuhakikisha kilimo kwanza kinafanyiwa kazi kwa uyakinifu ndiyo maana benki yetu tumeamua kusaidia katika suala hilo kwa asilimia 35,” alieleza.
Hata hivyo Dk, Kimei, alisema kuwa gharama za riba zimeongezeka kwa kipindi cha robo mwaka kutoka milioni 7,588 machi 2011 hadi kufikia milioni 13,515 katika kipindi cha machi mwaka huu ambayo ni sawa na asilimia 78.
Alisema kuwa mapato ya riba yameongezeka katika kipindi cha robo mwaka mwaka huu kwa asilimia 35 kutoka milioni 44,204 machi 2011 hadi milioni 59,543 .
Aliongeza kuwa kwa upande wa mapato halisi katika riba za amana na mikopo zimeongezeka kutoka milioni 36,616 kwa machi mwaka 2011 na kufikia milioni 46,028 kwa machi mwaka huu ambayo ni sawa na asilimia 26.
Habari & Picha na Francis Dande Blog
No comments:
Post a Comment