Tangazo

May 5, 2012

MAMA SALMA NA WAKE WA MAKAMU WA RAIS WATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA NETIBOLI YA TAIFA "TAIFA QUEENS"

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya netiboli,Taifa Queens, wakati wakifanya mazoezi kwenye kambi yao iliyoko katika shule ya sekondari ya Philbert Bayi huko Kibaha wakati alipowatembelea tarehe 4.5.2012.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mazoezi ya timu ya taifa huko Kibaha walikopiga kambi yao.
 


Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Salma Kikwete, akiwapa somo la kucheza na kufunga magoli wakati alipowatembelea kwenye kambi yao ya mazoezi wakijiandaa kwa michuano ya Afrika itakayofanyika hapa nchini hivi karibuni.

Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete, akimkabidhi mchango wa shilingi milioni kumi, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, kwa ajili ya maandalizi ya timu ya taifa ya mchezo huo. Makabidhiano hayo yalifanyika huko Kibaha tarehe 4.5.2012 ambako timu hiyo imeweka kambi.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete, akifuatana na wake wa Makamu wa Rais,Zakhia (wa pili) na Asha Bilali (wa mwisho) wakiagana na wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli huko Kibaha tarehe 4.5.2011. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments: