Tangazo

May 7, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAWAZIRI WATEULE IKULU DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Adam Malima,  kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo Mei, 7, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, baada ya hafla ya kuapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ya kuwaapisha ilifanyika leo Mei 7, 2012 katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani- OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo Mei, 7, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA Zitto Kabwe kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam, leo Mei 7, 2012 wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri wapya wateule. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwapongeza baadhi ya Mawaziri na Manaibu baada ya kuapishwa wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo Mei 7, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi, wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wateule baada ya kuapishwa rasmi leo Ikulu Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Rais Kikwete akimuapisha Amos Makala kuwa  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Rais Kikwete akimuapisha Dk. Fenela Mukangala kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Rais Kikwete akimuapisha Bi. Janet Mbene kuwa  Naibu Waziri wa Fedha.

Rais Kikwete akimuapisha January Makamba kuwa  Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano.

Rais Kikwete akimuapisha Dk. Harrison Mwakyembe kuwa  Waziri wa Uchukuzi.

No comments: