Arusha, Julai 6, 2012 (FH)
Wakati viongozi wa Chombo cha Umoja wa Mataifa kitakachorithi kazi za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari yaRwandawakiahidi kuwasaka watuhumiwa wakuu wa mauaji hayo,Libyawiki hii iliwaachia huru wafanyakazi wanne wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai waliokuwawanashikiliwa tangu Juni 7, 2012.
ICTR
Mrithi wa ICTR aanza kazi: Akizungumza katika uzinduzi wa Chombo cha Umoja wa Mataifa kitakachorithi kazi za ICTR, Rais wa Chombo hicho, Jaji Theodor Meron Jumatatu wiki hii aliahidi kuendelea kuwasaka watuhumiwa wakuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. Kwa upande wake Mwendesha Mashitaka Hassan Bubacar Jallow, alisema ofisi yake ipo tayari kuanza kushughulikia changamoto kuu ya Chombo hicho ambayo ni kuwasaka watuhumiwa hao.
Watuhumiwa wanaosakwa vikali ni pamoja na FĂ©licien Kabuga, anayedaiwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji hayo, Protais Mpiranya, ambaye alikuwa Kamanda wa kikosi cha walinzi wa Rais na Augustin Bizimana, Waziri wa zamani wa Ulinzi.
Bagosora apelekwa Mali: Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari yaRwanda imemhamishia nchini Mali Kanali Theoneste Bagosora kwenda kutumikia kifungo chake pamoa na wafungwa wengine watatu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano wiki hii, wafungwa wengine saba wamehamishiwa nchiniBenin kwa madhumuni kama hayo.
Awali, Bagosora, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Baraza katika Wizara ya Ulinzi nchiniRwanda alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. Hata hivyo, kifungo hicho kilipunguzwa hadi miaka 35 jela baada ya kukata rufaa.
RWANDA
Wafaransa watua Kigali kufanya uchunguzi: Ujumbe wa Kifaransa ambao umejikita katika makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu umewasili jijini Kigali Jumatano wiki hii kwa ajili ya kufanya uchunguzi.
Ujumbe huo utakutana na Mwandesha Mashitaka Mkuu pamoja na wakuu wa kitengo cha kuwasaka watuhumiwa wa mauaji ya kimbari. Kuna kesi takribani 20 nchini Ufaransa zinazowahusu Wanyarwanda wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mwaka 1994.
ICC
Libya yawaachia wafanyakazi wa ICC: Mamlaka nchini Libya Jumatatu wiki hii iliwaachia huru wafanyakazi wanne wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai waliokuwa wanashikiliwa tangu Juni 7, mwaka huu. Rais wa mahakama hiyo, Jaji Sang-Hyun Song amepongeza uamuzi huo, kwani utawawezesha wafanyakaizi hao kuungana na familia zao.
Wafanyakazi hao walikamatwa walipoenda kumtembelea Saif Al-Islam Gaddafi anayeshitakiwa na mahakama hiyo kwa uhalifu dhidi ya binadamu.
WIKI IJAYO
Lubanga kuhukumiwa: Jumanne ijayo, Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai itatoa adhabu dhidi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, Thomas Lubanga, ambaye ameshatiwa hatiani kwa makosa ya uhalifu wa kivita kwa kuwasajili na kuwatumia watoto kwenye vita katika Wilaya ya Ituri nchini humo kati ya Septemba 1, 2002 na Ogasti 13, 2003.

No comments:
Post a Comment