Tangazo

July 4, 2012

Vodacom yapongeza Vyombo vya Habari Sabasaba

• Yatumia milioni 120 kuboresha maonyesho ya sabasaba.
 
• Yapata Tuzo ya mdhamini rasmi wa mawasilaiano.

Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania imetumia zaidi ya milioni 120 katika kuboresha sekta ya mawasiliano katika maonyesho ya sabasaba ambapo fedha hizo zinatumika katika kuwezesha mawasiliano na machapisho mbalimbali katika maonyesho hayo.
 
Akizungumza na waandishi wa  habari mapema baada ya kukabidhiwa Tuzo ya udhamini wa maonyesho hayo, Mkuu wa mawasiliano na masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema kuwa fedha hizo zinatumika katika kuzalisha machapisho na mawasiliano kwa vyombo vya habari katika maonyesho hayo.

“Tunatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kutangaza maonyesho haya ya Kimataifa ya sabasaba kwani yanakusanya watu wengi kutoka sehemu mbalimbali na vyombo vya habari vinao mchango mkubwa katika kutoa taarifa kwa Watanzania ndio maana tumeamua kuwekeza kiasi hiki cha pesa katika kuhakikisha masuala yote ya mawasiliano yanafanyika vizuri ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa katika maonyesho haya,” alisema Kelvin na kuongeza, “Sisi kama wadhamini rasmi wa sekta ya mawasiliano tuliingia katika ushirikiano na Tantrade katika kuboresha sekta ya mawasiliano na tumewekeza zaidi ya milioni 120 katika kuboresha maonyesho haya ya sabasaba na fedha hizo zimelenga kutumika katika kuboresha maonyesho haya hasa katika sekta ya mawasiliano na mahusiano na vyombo vya habari.”

Katika uzinduzi wa maonyesho hayo yaliyofunguliwa na makamu wa pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddy, kampuni ya Vodacom Tanzania ilipata Tuzo ya mdhamini wa kwanza wa maonyesho hayo katika sekta ya mawasiliano. 

Maonyesho ya sabasaba yanayodumu kwa siku kumi hukusanya watazamaji zaidi ya 350,000 na kutoa fursa kwa watazamaji  kulinganisha ubora wa bidhaa na kufanya manunuzi.

No comments: