Tangazo

July 4, 2012

NHIF Nyanda za Juu kutumia Takukuru

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, umesema utatumia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili kubaini halmashauri ambazo zinafuja fedha zake.

Akizungumza mjini hapa, Meneja wa kanda, Celestin Mganga, alisema kuna mchezo mchafu unaofanywa kwa baadhi ya halmashauri kuandika hundi nyingi kwa malengo la kukomoa mfuko na kwamba, hawatavumilia hali hiyo na watahakikisha wanafuatilia kwa umakini.

“Hatutoweza kuvumia mchezo huo, lazima sasa tutumie Takukuru ili kudhibiti hali hiyo, kwani ina lengo mabaya tunajikuta hatuna wateja wengi na wananchi kutojua maana ya mradi huo,” alisema Mganga.

Pia, Mganga aliagiza waratibu wa NHIF kutoa elimu zaidi kwa wananchi hususan vijijini kujiunga na mfuko huo, ili kuwarahisishia upatikanaji huduma za afya kwa urahisi katika zahanati na vituo vya afya.

“Kumekuwapo na changamoto nyingi hususan wananchi kutokuwa na mwamko wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya, hivyo kuna ulazima wa waratibu kuingia vijijini zaidi ili kupata wateja wengi zaidi,” alisema. Chanzo: Gazeti la Mwananchi Julai 03.12

No comments: