Tangazo

August 30, 2012

BREAKING NEWS: MAMA HAWA NGULUME AMERARIKI DUNIA


Taarifa tulizozipata hivi punde ni kuwa aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali kwa vipindi tofauti Bibi Hawa Ngulume amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Kwa kujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatoilewa baadaye.

Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu .

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahali pema peponi, AMEN.
Mama Hawa Ngulume (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (kulia)  na John Guninita ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments: