Tangazo

August 30, 2012

Polisi yawakamata Wahalifu 126 wa kundi la Mungiki

Kamanda wa Polisi mkoa wa  kinondoni Charles Kinyela akiwaonyesha wandishi wa Habari silaha za jadi ikiwemo pinde na mishale ,mikuki, Mapanga na kadhaa zilizo kuwa zinatumiwa na watu wanaodaiwa wavamizi wa mashamba ya watu yaliyopo eneo la Madale.
*****************************

JESHI la Polisi Wilaya ya Kinondoni limefanikiwa kuwakamata wavamizi 126 wa kundi la Mungiki, lililokuwa linafanya uhalifu katika maeneo mbalimbali na kati yao, 10 si raia wa Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema Agosti 22, mwaka huu, walifanikiwa kufanya operesheni ya kuondoa wavamizi wa mashamba, viwanja, nyumba na maeneo ya wazi.

Alisema kati ya maeneo hayo ni Kinondo, Nakasangwe, Kazaroho, Mbopo, Boko Magereza na Benako Salasala.

“Tumefanikiwa kuwakamata wahalifu 126 waliokuwa wanatusumbua kwa muda mrefu ambapo 10 si raia wa Tanzania na wengine tumewafikisha mahakamani.

“Wavamizi hao walikuwa wamevamia maeneo kinyume na sheria kwa kuwa yalikuwa ni maeneo ya wananchi halali wa maeneo hayo,” alisema Kenyela.

Alisema wavamizi hao walikuwa na silaha za jadi kama mishale 22, mapanga, shoka moja, vipande vya nondo maarufu kama saba, upinde tisa, visu, marungu na mikuki.

“Wavamizi walikuwa wamejipanga kupigana na Jeshi la Polisi kwa kuwa walimrushia askari mshale wa tumboni lakini haukumdhuru kutokana na mavazi maalumu ya kujikinga na silaha.

“Jeshi letu lilikuwa limejipanga vya kutosha kuwakamata wavamizi waliokuwa wamevamia maeneo hayo. Katika operesheni yetu tuliweza kukamata pombe haramu lita 315, mitambo sita ya kutengenezea pombe hiyo na kilo 105 za bangi.

“Vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na mihuri bandia ya kuuzia viwanja na kutambulishana kuhusu maombi ya uraia kuhusu viongozi batili wa wavamizi waliokuwa wakijifanya kuwa ni viongozi wa Serikali za Mitaa, karatasi zenye ajenda za vikao vyao vya kupinga operesheni, Katiba na vitu vingine mbalimbali,” alisema Kenyela.

Katika tukio jingine, alisema kwa sasa Kinondoni iko shwari kutokana na doria na misako inayoendelea katika wilaya zote, kuanzia Agosti Mosi hadi jana jumla ya majambazi 20 wa kutumia silaha wamekamatwa.

Alisema majambazi hao walikamatwa bastola aina ya Glock 25 na Browning, risasi 46 zote za bastola, funguo bandia 118, nondo nne za kuvunjia maarufu kwa jina la saba.

No comments: