Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Winfrida Beatrice Korosso kuwa
Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini.
Taarifa iliyotolewa
leo, Jumatano, Agosti 22, 2012 mjini Dar
es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni
Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi
huo ulianza Agosti 14, mwaka huu, 2012.
Kabla ya uteuzi wake,
Bibi Korosso alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mkurugenzi wa Mashtaka
katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
22 Agosti,
2012
No comments:
Post a Comment