Bondia Kalama Nyilawila akipima uzito. |
MIAMBA ya masumbwi nchini, Bingwa wa Mabara Francis Cheka 'SMG' na aliyekuwa Bingwa wa Dunia, Karama Nyilawila 'Captain' wanatarajia kupanda ulingoni Jumamosi mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila walitwangana mbambanmo wao uliofanyika mkoani Morogoro hata hivyo ulizua utata baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambapo Cheka aliibuka na ushindi wa pointi .
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo, Oswald Mlay alisema pambano hilo litapigwa katika Ukumbi wa PTA uliopo ndani ya Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa wa Julius Nyerere (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini.
.
Alisema pambano hilo litakuwa la Raundi 12 uzito wa Kg 72 ambapo leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano huo utakaoamua nani zaidi.
Katika Mchezo huo pia DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitauzwa kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

No comments:
Post a Comment