Tangazo

September 20, 2012

MIKUTANO YA KATIBA KATAVI - LINDI NA ZIARA YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI TUME DAR

Bw. Amir Hashim Mkumba (57) mfanyabiashara, mkazi  wa mtaa wa Makanyagio, Kata ya Makanyagio, Wilaya ya Mpanda, mkoani  Katavi  akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani humo hivi karibuni.

Bw.Michael Elias Ndabi (21) mkazi  wa mtaa wa Makanyagio, Kata ya Makanyagio, Wilayani  Mpanda, mkoani  Katavi  akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani humo hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Bw. George Mwakajinga (58) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mjini Lindi hivi karibuni.

Askari Polisi wa mkoani Lindi Bi. Happyfania Gibson (24) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba hivi karibuni wilyani humo.

Wananchi wa kijiji cha Mihumo, wilayani Lindi wakifuatilia mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba hivi karibuni ili kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.

Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga (kulia), akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar majukumu ya Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) wakati walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Tume jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa tatu kulia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Ali Abdallah Ali na wa pili kulia ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaye pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Ali Abdalla Ali (wa tatu kulia). Wajumbe wa Kamati hiyo walifanya ziara katika Makao makuu ya Tume hivi karibuni. Wengine katika picha ni Mjumbe wa Tume, Waziri Mkuu mstaafu Dkt. Salim Ahemd Salim (kushoto).

No comments: