Tangazo

September 3, 2012

PICHA ZA MBWA MWITU WAKILA CHAKULA CHA MWISHO KABLA YA KUACHIWA HURU MBUGANI SERENGETI


Mbwa mwitu kumi na Moja wakipata mlo wao wa mwisho kabla ya kurudishwa mbugani siku ya Alhamisi Agosti 30, 2012  baada ya kuhifadhiwa kwenye boma maalumu la mradi unaojulikana kama Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project,  katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Jamii cha kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Bw. Yesaya Mwakifulefule akiangalia Mbwa mwitu kumi na Moja wakipata mlo wao wa mwisho kabla ya kurudishwa mbugani siku ya Alhamisi Agosti 30, 2012  baada ya kuhifadhiwa kwenye boma maalumu la mradi unaojulikana kama Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project,  katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom hapa nchini Bw. Rene Meza, Ikulu  Dar-Es-Salaam, walipokutana jana jioni, Ijumaa Agosti 31,2012, ambapo aliishukuru kampuni hiyo ya simu za mkononi kwa kuchangia katika mradi wa kuhifadhi mbwa mwitu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mradi unaojulikana kama Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project, kwa dola za Marekani 450,000 kwa kipindi cha miaka mitatu. kumi na Moja, wamerudishwa mbugani siku ya Alhamisi Agosti 30, 2012  baada ya kuhifadhiwa kwenye boma maalumu la mradi huo,  katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

No comments: