Tangazo

September 10, 2012

WIKI YA USALAMA BARABARANI: Serengeti Breweries Ltd yatoa Msaada wa Fulana 1000 na Vipeperushi 500

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga akipokea msaada wa fulana 1000 za kuhamasisha wiki ya usalama barabarani na vipeperushi 500   kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye makao makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti, Nandi Mwiyombela. Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 17.5 na kampuni hiyo imesema inaangalia uwezekano wa kuchapisha vipeperushi vingine kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam ambapo hivi vya awali vitapelekwa mikoani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga akipokea msaada wa vipeperushi 500 kwa ajili ya kuhamasisha wiki ya usalama barabarani kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika mkwenye makao makuu ya Trafic jijini Dar es salaam, kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti Nandi Mwiyombela.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga akizungumza katika makabidhiano hayo. Kulia kwake ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya SBL,Teddy Mpunda na Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti Nandi Mwiyombela.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mpunda akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo. Kulia kwake ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela. Mapichaz kwa Hisani ya Fullshangwe Blog

No comments: