Tangazo

October 8, 2012

Airtel Tanzania na Msanii AY waanza kampeni za kusaidia shule nchini

Wafanyakazi wa Airtel na Balozi wao Ambwene Yesaya  wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sinza Maalum iliyopo jijini Dar Es Salaam walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii kama mwendelezo wao wa kusaidia jamii kwa watoto wenye mahitaji maalum kupitia mradi wao wa kuchangia Elimu  kwa kushirikiana na BAMVITA.

Mwananafunzi wa shule ya Sinza Maalum akiimba wimbo wa mwanamuziki, Ambwene Yesaya 'AY' (wa tatu kutoka kulia), alipowatembelea mwishoni mwa wiki hii akiongozana na wafanyakazi wa Airtel. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Jamii  wa Airtel, Hawa Bayumi na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
********
Na Mwandishi wetu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii imeanza mchakato wa kutembelea baadhi ya shule zitakazonufaika na mradi maalum wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ili kujionea changamoto zinazowakabili pamoja na kuwahimiza watanzania kuweza kuchangia mradi huo unaoendeshwa kwa ushirikiano na Baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania (BAMVITA).

Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake msanii Maarufu AY itatembelea shule zote zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubaiunisha matatizo wanaoyokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia. Amesema shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum zinahitaji vitendea kazi vingi ili kuwafanya wanafunzi hao kuweza kupatiwa elimu inayostahili.

“Shule hizi zinamahitaji mengi sana, Airtel tumeona ni vyema kumtumia pia Balozi wetu huyu msanii maarufu nchini A Y kuendea kuwafikishia jamiii ujumbe waendelee kuchangia katika mradi huu wenye lengo la kuendeleza jamii” alisema Bi DANGIO KANIKI Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel
Akizungumza mara baada ya kutembelea shule ya msingi Sinza  Maalum Balozi wa Airtel AMBWENE YESAYA (A.Y) amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.

“Watoto hawa wenye uhitaji maalum nimejionea mwenyewe kuwa wakiwezeshwa wanaweza, ndio maana naona ni vyema zaidi kushirikiana na Airtel pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha tunawachangia vijana wetu hawa nao waweze kuendeleza hata vipaji vyao pamoja na elimu yao  .

Ninaomba kuwakubusha watanzania kuchangia katika kuwapatia vijana hawa vifaa mbalimbali ambavyo ni changamoto kwao, unaweza kuchangia kwa kupitia  Airtel Money ambapo unaandika jina la fumbo VITABU na utatuma kiasi chochote au kwa kutuma SMS yenye neno VITABU kwenda namba 15626 na atakuwa amechangia shilingi 200 tu.

Watanzania naomba tusaidiane katika elimu kwa kuwa tuanaamini Tanzania itajengwa na sisi wenyewe. Alimalizia kusema  Ambene Yessaya Balozi wa Airtel .

Wakati wa ziara hiyo mwishoni mwa wiki hii Mwalimu Mkuu wa shule ya Sinza Maalum, Simon Milobo alibainisha kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia pamoja na mafuta ya kuendeshea gari la wanafunzi.

Kampeni ya Airtel kwa kushirikiana na Bamvita itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na Watanzania wataweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 itakayoingizwa katika mradi huu”

No comments: