Tangazo

October 31, 2012

Barclays yazindua ofisi za kitengo cha ukusanyaji na ugomboaji madeni

Benki ya Barclays Tanzania imefanya hafla ya kuzindua kitengo chake cha Ukusanyaji na ugomboaji wa madeni ya mikopo katika jengo la Peugeot jijini Dar es Salaam juzi. Kabla ya hapo kitengo hicho kilikuwa katika Tawi la benki hiyo la Barabara ya Uhuru. Pichani Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Kihara Maina (katikati) pamoja na uongozi wa juu wa benki hiyo nchini (CMC Members) wakikata keki kuashiria uzinduzi huo jijini Dar es Salaam. Sasa wateja wanaweza kuhudumiwa katika jengo hilo badala ya Tawi la Uhuru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Kihara Maina (katikati) akikata utepe kuashiria  uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina (katikati), viongozi wa juu wa benki hiyo nchini (CMC Members) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Ukusanyaji na Ugomboaji wa madeni ya mikopo, wakipozi kwa picha katika hafla ya uzinduzi wa idara hiyo katika jengo la Peugeot jijini Dar es Salaam jana.

No comments: