Sheikh Farid akipokelewa na familia yake baada ya kurejea nyumbani kwake jana jioni. |
Sheikh Farid akiwa na wanawe baada ya kurejea nyumbani kwake jana jioni. |
Akiswali na Masheikh wenzake baada ya kurudi. |
***************************************
Baada ya kutoweka tangu siku ya Jumanne Oktoba 16.2012, hatimaye Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Farid amepatikana Ijumaa Oktoba 19.2012 jioni.
Akizungumzia yaliyomsibu kwenye mahojiano, Sheikh Farid alisema kwamba alichukuliwa na watu walio jitambulisha kama askari polisi kwa kuonyesha vitambulisho vyao, baadhi yao walikuwa na silaha.
Akizungumzia yaliyomsibu kwenye mahojiano, Sheikh Farid alisema kwamba alichukuliwa na watu walio jitambulisha kama askari polisi kwa kuonyesha vitambulisho vyao, baadhi yao walikuwa na silaha.
Walimchukua kwenye gari na kumfunga kitambaa usoni kisha kumpeleka kwenye nyumba asiyoitambua.
Amedai askari hao wenye lafudhi za Bara na wengine Visiwani, walitaka kujua kuhusu harakati zake zikiwemo safari zake za nje zikiwemo za Uarabuni na mahusiano yake na baadhi ya viongozi wa serikali.
Amedai askari hao wenye lafudhi za Bara na wengine Visiwani, walitaka kujua kuhusu harakati zake zikiwemo safari zake za nje zikiwemo za Uarabuni na mahusiano yake na baadhi ya viongozi wa serikali.
Pia askari hao walichukua simu yake na kumuhoji mengi kuhusu namba na message zilizopo kwenye simu yake.
Alisema watu hao waliomchukua kwa gari walikuwa wanne, akiwepo dereva na mwingine aliyekaa mbele ambaye alijitambulisha kwake, na nyuma ya gari walikuwepo watu wawili waliovaa kofia zilizofunika nyuso zao.
Kwa masaada wa mtandao
No comments:
Post a Comment