Na Evelyn Mkokoi
Doha
Utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji ya kupunguza hewa ukaa na uharibifu wa misitu (MKUHUMI) ulenge kunufaisha wananchi na nchi katika maeneo husika
Tanzania imesema kuwa, mfumo wa utoaji fedha kwa ajili ya kupunguza utoaji wa gesijoto na uharibifu katika sekta ya misitu hususan kwa nchi zinazoendelea unatakiwa uwe wenye manufaa kwa nchi na wananchi katika maeneo husika.
Hayo yameelezwa leo na Bwana Freddy K. Manyika, Afisa Misitu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, katika majadiliano kuhusu Mfumo wa Ufuatialia na Utaratibu wa utoaji wa fedha, yanayoendelea katika mkutano wa 18 wa nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchia unaofanyika mjini Doha, Qatar.
Akiwasilisha msimamo huo wa Tanzania, bw. Manyika ameleeza kuwa,Kuwepo kwa mfumo bora na wa ufuatialiaji na utoaji wa fedha utatoa motisha kwa uhifadhi na usimamizi endelevu katika sekta ya misitu kwa nchi maskini..
Akizungumza kwa niaba ya nchi zinazoendela (Least developed Countries -LDCs) Bw. Manyika alisema kuwa maisha ya wananchi katika nchi zinazoendelea husuan nchi maskini yanategemea sekta ya misitu kwa ajili ya kupata nishati, chakula, madawa, ujenzi wa makaazi na miundombinu, malisho ya mifugo, shughuli za kitamaduni, utalii, na huduma mbalimbali za kijamii kwa kiwango kikubwa, hivyo kwa kuzingatia umuhimu huo, mfumo wa ufuatilaiji na utaratibu wa malipo unaoandaliwa kwa ajili ya kusaidia sekta ya misitu hauna budi kutoa malipo yenye manufaa na motisha kwa wananchi wanaotunza misitu badala ya kutaka kutoa mwanya kwa makampuni ya kibiashara yenye mitaji mikubwa kunufaika na rasilimali hiyo.
“Tanzania na nchi zinazoendelea hazikubaliani na mfumo unaolenga kuwafanya wananchi wanaozungukwa na kutunza misitu hiyo kwa miaka mingi kugeuzwa vibarua na wapakazi katika makampuni yenye lengo la kujinufaisha kwa kutumia rasilimali na nguvu za wananchi maskini, Alisisitiza.”
Aidha Bw. Manyika aliongeza kuwa, kufikiwa kwa makubaliano kuhusu mfumo na utaratibu wa utoaji wa fedha kwa ajili ya shughuli za MKUHUMI katika mkutano wa Doha utasaidia kurejesha motisha kwa wananchi kuhifadhi misitu katika maeneo yao na hivyo kuendeleza shughuli za utunzaji mazingira na kuchochea maendeleo na uhifadhi endelevu kupitia sekta ya misitu.
Katika majadiliano yanayoendelea hapa mjini Doha, nchi wanachama wanatakiwa kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na utaratibu wa utoaji wa fedha kwa shughuli za upunguzaji wa gesijoto na utunzaji wa misitu ili kupunguza uharibifu. Mkutano wa 18 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unafanyika Doha, Qatar, kuanzia tarehe 26 Novemba hadi 7 Desemba 2012.

No comments:
Post a Comment