KAMPUNI ya MultiChoice imeandaa kwa mara ya pili tuzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari na wa elimu ya juu kutoka barani Afrika zijulikanazo kama DStvEutelsat Star Awards.
Tuzo hizi zitatolewa baada ya kufanyika mchuano mkali wa wanafunzi zaidi ya 1000 katika shule mbalimbali za Afrika nzima, shindano hilo la tuzo limeandaliwa na MultiChoice kwa kushirikiana na Eutelsat Communications.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kanda ya Afrika wa Eutelsat Joaquim Pereira de Lima, akizungumza Dar es Salaam, alisema kuwa kwa mara ya pili sasa tuzo hizo zinatolewa kwa wanafunzi ambao wamefanya vizuri kitaaluma.
Alisema mashindano hayo kwa mwaka huu, yamefikia katika hatua nzuri na kwamba tayari washiriki watakaoshindana siku ya fainali kwa ajili ya tuzo hizo wameshapatikana.
Lengo la mashindano hayo ambayo washindi watapata tuzo, ni pamoja na kuongeza msukumo wa kufikiria jinsi changamoto ya ukuaji wa teknolojia unavyoweza kuisaidia Afrika kwa baadaye.
Tuzo hiyo kwa mwaka huu, imepiga hatua kwani hata jopo la majaji wameongezeka ambapo linajumuisha wasomi na wafanyabiashara wakubwa.
Miongoni mwao ni mwanaanga wa kifaransa Patrick Baudry, ambaye alizaliwa Douala, Cameroon. Huyu tayari amekubali mwaliko wa MultiChoice na ndiye atakuwa mwenyekiti wa jopo kwa ajili ya tuzo za Eutelsat kwa mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya jopo hiyo, Baudry anasema wako tayari kuhakikisha wanasaidia kukuza maendeleo ya vipaji vya vijana, ambavyo vitasaidia kuzifanya akili zao zifanye kazi zaidi ili waweze kufikia malengo yao waliyojiwekea.
"Tunaangalia mbele zaidi katika kuboresha mawazo na ubunifu, hususan kwa kuwawezesha kufikiria zaidi, ambapo siku ya fainali, Novemba 22, mwaka huu, jijini Dar es Salaam watakapoonesha uwezo wao, ambapo zawadi kwa mshindi wa tuzo itatolewa," alisema Baudry.
Kwa mara ya kwanza tuzo za nyota wa DStvEutelsat, zilichukuliwa na Mary Musimire kutoka nchini Uganda ambaye aliibuka mshindi baada ya kuandika andiko lililokuwa bora zaidi ya wengine. Naye Michael Yeboah kutoka Ghana alikuwa mshindi wa pili, kwa sasa wanaendeleza ubunifu wao barani Afrika.
"Kimsingi ni kwamba tumezungukwa na vipaji vingi, kwa sasa tunaona namna vinavyozidi kupatikana baada ya kuanzishwa kwa shindano hili. Hivyo tunaipongeza MultiChoice pamoja na Eutelsat Communications, ambao wamekuja na shindano hili kwa ajili ya kuibua vipaji barani Afrika.
"Hivyo tunataka kuona ubunifu wa mshindi wa pili mwaka jana, Michael Yeboah na washindi wengine watakaopatikana mwaka huu zikienda angani kwa kutumia roketi ya Ariane ikiruka kwa kutumia satilaiti," alisema Mkurugenzi wa Masoko wa Kanda ya Afrika wa Eutelsat Joaquim Pereira de Lima.
Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda ya Afrika Mashariki, Stephen Isaboke ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo, akizungumza Dar es Salaam, alisema "Kuna faida kubwa tuzo hizi kutolewa Tanzania.
"Si tu ni mafanikio pekee, bali pia ni katika kuinua vipaji vya vijana na kufurahia wenyewe kama Waafrika na kuonesha mchango wetu tunaoweza kuufanya sehemu nyingine duniani," alisema Isaboke.
Alisema kuwa itakuwa bahati ya kipekee katika siku ya utoaji tuzo, ambapo nyota wawili wa kiafrika watakapopata nafasi ya kuliwakilisha Bara la Afrika ulimwenguni watakapokwenda kujionea roketi na kutembelea makao makuu ya ofisi za Eutelsat sanjari na vifaa vya satilaiti.
"Tunawatakia kila la heri wale wote waliongia fainali katika kipindi cha mwisho wa shindano hili," alisema.
Kuhusu Eutelsat Communications
Eutelsat Communications (Euronext Paris: ETL, ISIN code: FR0010221234), ni kampuni tanzu ya Eutelsat ya Afrika Kusini, imeunganishwa na satilaiti 29, inatoa huduma katika Bara la Ulaya, Mashariki ya Kati, Afrika na katika baadhi ya sehemu barani Asia na America.
Eutelsat ni kati ya kampuni tatu zinazoongoza katika uendeshaji wa satilaiti duniani. Hadi Septemba 30, 2012, Satilaiti za Eutelsat zilikuwa zinahudumia zaidi ya channeli 4,400 za televisheni, ambapo ni zaidi ya kebo milioni 200 barani Afrika, Ulaya na Mashariki ya Kati.
Pia satelaiti za Eutelsat zinahudumia eneo kubwa la huduma za mawasiliano ikiwamo ya simu, TV, network na katika utoaji wa huduma za intanenti na usafiri wa majini na angani.
Eutelsat inatoa huduma za intanenti zenye spidi kubwa kupitia mikonga yake iliyoko nchini Ufaransa, Italia ambapo huwawezesha wateja wake hususan wafanyabiashara, jamii, taasisi za serikali mashirika yanayotoa misaada Ulaya, Afrika, Asia na Marekani. Makao Makuu yake yapo Paris Ufaransa. Imeajiri watumishi wenye ujuzi zaidi ya 750 wakiwamo mafundi.
Watumishi hao wameajiriwa kutoka nchi 30. www.eutelsat.com

No comments:
Post a Comment