Tangazo

February 11, 2013

AIRTEL yatoa msaada wa sare na viatu kwa Wanafunzi wote wa Shule ya Msingi Koromo - Bagamoyo

 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki akimvalisha sare za shule na viatu mwananfunzi wa shule ya msingi Kiromo zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii.Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.

Meneja wa uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi sare za shule Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasib Pangahela  mwishoni mwa wiki hii, akishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii (katikati) bi Hawa Bayumi.

 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki  (Kulia) akimpongeza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kiromo (kulia) baada ya makabidhiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii wakishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi (wa pili kulia) akifuatiwa na mmoja wa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo bi Zuwena Salumu, Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.


Meneja wa uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi  mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kiromo sare za shule zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii, akishuhudia makabidhiano hayo (wa pili kushoto) meneja wa huduma kwa jamii bi Hawa Bayumi akifuatiwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasib Pangahela,  Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
######################
 Alhamisi 10 Februari 2013,  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa gharama nafuu zaidi Tanzania, leo imegawa sare za shule pamoja viatu katika shule ya msingi Kiromo iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Shule ya kiromo ni moja kati ya shule zilizofaidika na mpango wa shule yetu na kuingia kwenye ukarabati wa majengo na madarasa na kubadili mazingira ya shule na kutoa vifaa vya kufundishia pamoja na computer. sasa Airtel imetoa Sare na viatu vya shule kwa wanafunzi wote shuleni hapo.

Katika kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja shughuli za kijamii bi. Hawa Bayumi alisema” Airtel imedhamiria kuendelea kuisadia shule mbalimbali kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Na leo tunaendelea kuboresha shule yetu ya Kiromo kwa kutoa msaada wa uniform na viatu kwa wanafunzi.

M msaada wa sare zashule tunazoto ni pamoja na Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.

Airtel Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka na upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Leo tunathibitisha dhamira yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa sare za shule na viatu Kiromo shule ya msingi”, alisema Bayumi Airtel itaendelea kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na vifaa mbali mbali vya kufundishia ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia jamii, nia yetu ni kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania aliongeza.

Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini. Tangu tulipoanza mradi wa “ shule yetu” mpango wa  kusaidia vitabu na vifaa vya shule , shule mbalimbali nchini zimeshafaidika na mradi huu mpaka sasa.

No comments: